Uliteremshwa Wahyi kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa na umri wa miaka arobaini

Uliteremshwa Wahyi kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa na umri wa miaka arobaini

Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yao- amesema: Uliteremshwa Wahyi kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa na umri wa miaka arobaini, akakaa Makkah miaka kumi na tatu, kisha akaamrishwa kuhama, hivyo akahama kwenda Madina, akakaa Madina miaka kumi, kisha akafariki Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anaeleza Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: kuwa Wahyi uliteremshwa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na akatumwa akiwa na umri wa miaka arobaini, basi akakaa Makkah miaka kumi na tatu baada ya kuteremshiwa wahyi, kisha akaamrishwa kuhama kwenda Madina na akakaa huko miaka kumi, kisha akafariki -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa na umri wa miaka sitini na tatu.

فوائد الحديث

Maswahaba kuipa umuhimu historia ya Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake.

التصنيفات

Mtume wangu Muhammad - Rehma na amani za Allah ziwe juu yake-, Historia(Sira) ya Bwana Mtume.