na mimi ndiye ninaitwa Dhwamam Bin Thaalaba ndugu wa Banii Saad Bin Bakri

na mimi ndiye ninaitwa Dhwamam Bin Thaalaba ndugu wa Banii Saad Bin Bakri

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Wakati mmoja tulipokuwa tumekaa Msikitini pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliingia mtu mmoja akiwa juu ya Ngamia, akampigisha magoti Ngamia ndani ya Msikiti kisha akamfunga, kisha akawaambia Maswahaba: Kati yenu Muhammad ni nani? Na wakati huo Mtume -Rehema na mani ziwe juu yake- akiwa kati yao amekaa kwa kuegemea, tukasema ni huyu mtu mweupe aliyeegemea, yule mtu akamwambia: Ewe mtoto wa Abdul Muttwalib, basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akasema: "Nimekuitikia" Yule bwana akamwambia Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake- Hakika mimi nitakuuliza nanitatia mkazo katika kuuliza, hivyo usinichukie kwenye moyo wako, na wala usiona tabu kunijibu, akasema: "Uliza unachotaka" Akasema: Nanakuuliza kwa jina la Mola wako na Mola wa waliokuwa kabla yako, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekutuma kwa watu wote? Akasema: "Ndiyo, ni kweli" Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu ametuamrisha sisi tusali sala tano usiku na mchana? Akasema:"Ndiyo, ni kweli" Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha kuwa sisi tufunge Mwezi huu kila Mwaka? Akasema: "Ndiyo, ni kweli" Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha kuwa uchukue hizi sadaka kutoka kwa matajiri na uzigawanye kwa mafukara wetu? Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Ndiyo, ni kweli" Basi yule bwana akasema: Nimeamini yote yale uliyokuja nayo, na mimi ni mjumbe kuna wanaonifuata nyuma yangu, na mimi ndiye ninaitwa Dhwamam Bin Thaalaba ndugu wa Banii Saad Bin Bakri."

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anatoa habari Anas Bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Wakati mmoja Maswahaba walikuwa wamekaa pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Msikitini aliingia mtu mmoja akiwa juu ya Ngamia, basi akampigisha magoti kisha akamfunga Ngamia wake, Kisha akawauliza: Kati yenu Muhammad ni nani? Na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa amekaa kati ya watu na ameegemea, tukamwambia: Ni mtu huyu mweupe aliyeegemea, Yule bwana akamwambia: Ewe mtoto wa Abdul Muttwalib, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Nimekusikia, basi uliza nitakujibu. Yule bwana akamwambia Mtume -Rehema na mani ziwe juu yake-: Mimi nitakuuliza na nitakuuliza kwa msisitizo mkubwa hivyo usinichukie wala usione dhiki katika nafsi yako. Yaani: Usinikasirikie wala usione dhiki, Akasema: Uliza unachotaka, Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mola wako na Mola wa waliokuwa kabla yako, Je ni kweli Mwenyezi Mungu amekutuma kwa watu wote? Akasema: Ndiyo ni kweli, hali ya kutilia mkazo ukweli wake, Yule bwana akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha yakuwa sisi tusali sala tano usiku na mchana? Nazo ni sala za faradhi, Akasema: Ndiyo ni kweli, Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha yakuwa sisi tuufunge Mwezi huu katika kila Mwaka? Yaani Mwezi wa Ramadhan, Akasema: Ndiyo ni kweli, Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha kuwa uchukue hizi sadaka kutoka kwa matajiri wetu kisha uzigawe kwa mafukara wetu? Na sadaka hiyo ni Zaka, Basi akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-Ndiyo ni kweli, Basi Dhwamamu akasilimu, na akamwambia Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yeye atawalingania watu wake kuingia kwenye uislamu, kisha akajitambulisha kuwa yeye ni Dhwammam Bin Thaalabah atokanae na kabila la Banii Saad Bin Bakri.

فوائد الحديث

Unyenyekevu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa namna ambayo hakuweza mtu yule kumtofautisha kati ya Mtume na Maswahaba zake.

Uzuri wa tabia za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- upole wake katika kumjibu muulizaji, na kuwa kurudisha majibu mazuri ni miongoni mwa sababu ya kukubalika Daawa.

Inafaa mtu kujitambulisha kwa sifa ya rangi ya weupe au wekundu, na urefu na ufupi, na mfano wa sifa hizo ikiwa haikusudiwi kuaibisha, ikiwa msifiwa hatochukia sifa hizo.

Yafaa kwa Kafiri kuingia Msikitini kwa haja maalumu.

Haikutajwa Hijja katika hadithi kwa sababu hueda ikawa Hijja ilikuwa haijafaradhishwa wakati wakuja kwake.

Pupa ya Maswahaba ya kuwalingania watu; Basi kwa muda mfupi tu baada ya kusilimu kwake alikuwa na pupa ya kuwalingania watu wake.

التصنيفات

Kumuamini Allah mwenye nguvu alie tukuka, Mtume wangu Muhammad - Rehma na amani za Allah ziwe juu yake-, Uislamu, Kulingania na kuelekeza kwa Mungu., Wajibu wa Swala na Hukumu ya Mwenye kuiwacha., Wajibu wa Zakkah na Hukumu ya Mwenye kuiwacha.