إعدادات العرض
Vaeni katika nguo zenu nguo nyeupe, kwani hizo ni katika nguo zenu bora, na wavisheni kwazo maiti wenu
Vaeni katika nguo zenu nguo nyeupe, kwani hizo ni katika nguo zenu bora, na wavisheni kwazo maiti wenu
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Vaeni katika nguo zenu nguo nyeupe, kwani hizo ni katika nguo zenu bora, na wavisheni kwazo maiti wenu".
[Sahihi]
الترجمة
العربية Tiếng Việt Bahasa Indonesia Nederlands অসমীয়া English ગુજરાતી සිංහල Magyar ქართული Hausa Românăالشرح
Anawaelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake wanaume kuvaa nguo zenye rangi nyeupe na kuwavisha maiti pia; kwani ni katika nguo bora.فوائد الحديث
Sunna ya kuvaa nguo nyeupe, na inafaa pia kuvaa rangi nyingine tofauti na hiyo.
Sunna ya kuwavisha maiti nguo nyeupe.
Amesema Shaukani: Na hadithi inaonyesha sheria ya kuvaa nguo nyeupe na kuwavisha nazo maiti pia; kwakuwa ni safi zaidi na ni nzuri zaidi, ama kuwa kwake ni nzuri hili liko wazi, na ama kuwa kwake ni safi ni kwa sababu kitu chochote hata kikwa kidogo kikidondokea juu yake huonekana, ndio maana inapendekezwa.
التصنيفات
Adabu za kuvaa.