Tambueni kuwa pombe imekwisha haramishwa

Tambueni kuwa pombe imekwisha haramishwa

Imepokewa kutoka kwa Anas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake amesema: Nilikuwa nikihudumia watu vinywaji katika nyumba ya Abuu Twalha, na pombe yao wakati huo ilikuwa ni mchanganyiko, akaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kunadi akanadi: Tambueni kuwa pombe imekwisha haramishwa, akasema: Abuu Twalha akasema kuniambia: Toka, nenda kaimwage, nikatoka nikaimwaga, ikatiririka pombe mitaro ya Madina, baadhi ya watu wakasema: Wameuliwa baadhi ya watu na pombe ikiwa tumboni mwao, Mwenyezi Mungu akateremsha: "Hapana ubaya kwa wale walioamini na akafanya matendo mema katika vile walivyokula" [Al-Maaida: 93] Mpaka mwisho wa aya.

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Ameeleza Anas bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba alikuwa akitoa huduma ya vinywaji (pombe) kwa wale waliokuwa katika nyumba ya mume wa mama yake Abuu Twalha radhi za Allah za ziwe juu yake, na pombe yao wakati huo ilikuwa ni mchanganyiko, kati ya tende mbivu na tende mbichi, ghafla mnadiji wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akanadi: Tambueni kuwa pombe imekwisha haramishwa, akasema: Anasema: Abuu Twalha akasema kuniambia, toka nenda kaimwage na uimimine, nikatoka nikaimwaga na nikaimimina, pombe ikatiririka katika mitaro ya Madina, wakasema baadhi ya watu: Wameuliwa baadhi ya Maswahaba na pombe ikiwa tumboni mwao ikiwa bado haijaharamishwa, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hapana ubaya kwa wale walioamini na wakafanya matendo mema katika yale waliyokula". [Al-Maaida: 93] Mpaka mwisho wa aya. Yaani: Hawana dhambi wale walioamini katika vile walivyokula na kunywa katika pombe kabla ya kuharamishwa kwake.

فوائد الحديث

Ubora wa Abuu Twalha na Maswahaba wengine radhi za Allah ziwe juu yao, pale walipoitikia amri ya Mwenyezi Mungu kwa haraka bila kuuliza, na hivi ndivyo inavyotakiwa kwa muislamu wa kweli.

Pombe: Ni jina linalokusanya kila chenye kulewesha.

Fadhii: Ni kinywaji kinachotokana na tende mbichi na tende mbivu pasina kupikwa, na Busri: Ni matunda ya tende kabla hajaanza kuiva.

Amesema bin Hajari: Amesema Mulhib: Bila shaka pombe ilimwagwa barabarani ili kutangaza kuikataa kwake na kutangaza kuiacha kwake, na hili linakuwa na masilahi makubwa kuliko kukereka kwa kuimwaga kwake barabarani.

Kumebainishwa rehema ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na kwamba hawahesabu watu katika kitendo kabla ya kuteremsha hukumu.

Mwenyezi Mungu Mtukufu ameharamisha pombe; kwakuwa ndani yake kuna uharibifu ambao madhara yake yanarudi katika akili na mali, na kwa sababu yake mtu hutenda madhambi mengi; kwa kutoweka akili yake.

التصنيفات

Sababu za kuteremka aya, Vinywaji na vilivyoharamishwa.