إعدادات العرض
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiosha, au akioga, kwa kibaba kimoja mpaka vibaba vitano, na anatawadha kwa kibaba kimoja
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiosha, au akioga, kwa kibaba kimoja mpaka vibaba vitano, na anatawadha kwa kibaba kimoja
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiosha, au akioga, kwa kibaba kimoja mpaka vibaba vitano, na anatawadha kwa kibaba kimoja.
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt Hausa Kurdî Português සිංහල অসমীয়া አማርኛ ગુજરાતી Nederlands پښتو नेपाली ไทย മലയാളം Кыргызча Română Malagasyالشرح
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akioga janaba kwa kibaba kimoja mpaka vitano, na alikuwa akitawadha kwa kibaba kimoja. Na kibaba ujazo wake ni: mud nne, na mud moja ni: kiasi cha kujaza kiganja cha mtu mwenye mwili wa wastani.فوائد الحديث
Sheria ya kufanya bajeti katika maji ya udhu na kuoga, na kutofanya fujo, hata kama maji yatakuwa mengi na rahisi kupatikana.
Sunna ya kupunguza maji wakati wa udhu na kuoga, kulingana na uhitaji, nakuwa huu ndio muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Lengo ni kueneza maji katika udhu na kuoga ikiwa ni pamoja na kuchunga sunna na adabu pasina kufanya fujo wala ubahili, na muda uzingatiwe pia na wingi wa maji na uchache wake na mengineyo.
Janaba huitwa kwa kila aliyeshusha manii au kafanya tendo la ndoa, na limeitwa hivyo kwa sababu ya mwenye janaba kujiweka mbali na swala na ibada zingine mpaka awe msafi.
Kibaba ni: Kipimo maarufu, na makusudio yake ni kibaba cha Mtume, na kinafikia uzito wake gram (480) za ngano safi, na kwa lita ni lita tatu (3)
Mud: Ni ni kilo moja kisheria, nayo ni ujazo wa viganja viwili vya mtu mzima atakapovijaza na akanyoosha mikono yake, na Mud ni nusu ya kibaba, kwa itifaki ya wanachuoni wote, na kiwango chake ni mil (750).
التصنيفات
Sunna na Adabu za Kutawadha