إعدادات العرض
Hakika hastahiki kuadhibu kwa Moto isipokuwa Mola Mlezi wa Moto
Hakika hastahiki kuadhibu kwa Moto isipokuwa Mola Mlezi wa Moto
Kutoka kwa bin Masoud radhi za Allahi ziwe juu yake amesema: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, akaondoka kwa ajili ya haja yake, tukaona ndege akiwa na makinda mawili, tukawachukua makinda wake, akaja yule ndege akaanza kupepesa mbawa zake, basi akaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Ni nani aliyemuhuzunisha ndege huyu kwa mwanaye? Mrejesheeni mwanaye", na akaona kijiji cha wadudu chungu tulichokichoma kwa moto, akasema: "Hakika hastahiki kuadhibu kwa Moto isipokuwa Mola Mlezi wa Moto".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt සිංහල Hausa Kurdî Magyar ქართული Română অসমীয়াالشرح
Ameeleza Abdallah bin Masudi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba wao walikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, akaondoka rehema na amani ziwe juu yake kwa ajili kukidhi haja yake, Maswahaba zake wakapata ndege aina ya Hummara akiwa na makinda mawili, wakayachukua, yule ndege akaanza kupeperusha mbawa zake na kuzipepesa kwa huzuni kwa kuwakosa makinda wake, akaja rehema na amani ziwe juu yake na akasema: Ni nani aliyemuhuzunisha na akamuhofisha kwa kuchukua vitoto vyake? Kisha akaamrisha virejeshwe kwake. Kisha akaona kijiji cha wadudu chungu kilichochomwa kwa moto, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Ni nani aliyekiunguza hiki? Wakasema baadhi ya Maswahaba: Sisi. Akasema kuwaambia: Hakika haifai kwa yeyote kuadhibu kiumbe hai kwa moto; isipokuwa Mwenyezi Mungu muumba wake.فوائد الحديث
Sheria ya kujisitiri kwa ajili ya kukidhi haja.
Katazo la kuwaadhibu wanyama kwa kuchukua watoto wao.
Katazo la kuwachoma sisimizi na wadudu wengineo kwa moto.
Himizo la upole na huruma kwa wanyama, na Uislamu ndio ulitangulia kulisema hilo.
Huruma yake rehema na amani ziwe juu yake kwa wanyama.
Kuadhibu kwa moto ni miongoni mwa mambo anayohusika nayo Mola Mtukufu pekee.