Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mali zimeteketea na njia zote zimekatika, muombe Mwenyezi Mungu atuletee mvua

Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mali zimeteketea na njia zote zimekatika, muombe Mwenyezi Mungu atuletee mvua

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Ya kwamba mtu mmoja aliingia msikitini siku ya Ijumaa kupitia mlango uliokuwa upande wa Dar Al-Kadhaa, na huku Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesimama akihutubu, akamuelekea Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa wima, kisha akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mali zimeteketea na njia zote zimekatika, muombe Mwenyezi Mungu atuletee mvua, akanyanyua Mtume rehema na amani ziwe juu yake mikono yake, kisha akasema: "Ewe Mola wetu tunyeshelezee, Ewe Mola wetu tunyeshelezee, Ewe Mola wetu tunyeshelezee". Akasema Anasi: Namuapa Mwenyezi Mungu, hatukua tukiona mbinguni mawingu wala dalili, na kati yetu na Mlima Sal'i hapakuwa na nyumba wala makazi, anasema: Likachomoza wingu nyuma yake mithili ya ngao, lilipofika kati kati ya mawingu likatanda kote, kisha mvua ikaanza kunyesha, namuapa Mwenyezi Mungu hutukuliona Jua kwa muda wa siku , kisha akaingia bwana mmoja kupitia mlango ule ule siku ya Ijumaa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa wima akihutubia, akamuelekea akiwa kasimama akasema ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mali zimeangamia, na njia zimekatika, muombe Mwenyezi Mungu aizuie kwetu mvua, anasema akanyanyua Mtume rehema na amani ziwe juu yake mikono yake, kisha akasema: "Ewe Mwenyezi Mungu inyeshe pembezoni mwetu na si juu yetu, ewe Mwenyezi Mungu inyeshe katika vichuguu na milima na ndani ya mabonde, na katika maoteo ya miti" Anasema: Mvua ikakata, na tukatoka tukitembea juani, amesema Shariki: Nilimuuliza Anasi, je ni yule yule mtu wa kwanza? Akasema: "Sijui".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Aliingia bedui mmoja msikiti wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ya Ijumaa kupitia mlango wa Magharibi upande wa nyumba ya Omari bin Khattwab radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa kasimama anahutubia, yule bwana akamuelekea Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akasema, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wanyama wameangamia, na njia zote zimekatika kwa kufa mifugo inayobeba watu, au imedhoofika kutokana na njaa, basi muombe Mwenyezi Mungu atunyeshelezee mvua. Akanyanyua rehema na amani ziwe juu yake mikono yake, kisha akasema: Ewe Mwenyezi Mungu tunyeshelezee, Ewe Mwenyezi Mungu tunyeshelezee, Ewe Mwenyezi Mungu tunyeshelezee. Amesema Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake: Wallahi hatukua tukiona mbinguni hata kipande cha mawingu, na hapakuwa kati yetu sisi msikitini na Mlima Sal'i ulioko Magharibi mwa msikiti upande ambao hujia mawingu nyumba wala makazi yanayoweza kutuzuia kuona mawingu. Amesema Anasi radhi za Allah ziwe juu yake: Likatokeza nyuma yake wingu la duara mfano wa ngao nayo ni mviringo mdogo, lilipofika kati kati ya mawingu ya Madina likatanda, kisha mvua ikaanza kunyesha, na namuapa Mwenyezi Mungu, hatukuliona Jua tena kutokana na mvua mpaka Ijumaa iliyofuata, kiasi kwamba aliingia tena yule bwana kupitia mlango ule ule, huku rehema na amani ziwe juu yake akiwa kasimama anahutubia, akamuelekea akiwa wima, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mali zimeangamia na njia zimekatika, basi muombe Mwenyezi Mungu aizuie mvua kwetu. Akasema: Akanyanyua rehema na amani ziwe juu yake mikono yake, kisha akasema: Ewe Mwenyezi Mungu igeuze mvua iende pembezoni mwetu ewe Mwenyezi Mungu ielekee katika sehemu zenye miinuko katika Ardhi kama kichuguu, na milima midogo, na ndani ya mabonde, na maoteo ya miti. Akasema Anasi: Yakakatika mawingu ya mvua, na tukatoka tukitembea juani.

فوائد الحديث

Kufanya sababu za kutafuta riziki, kama kuomba dua, na kusafiri katika Ardhi, hakupingani na kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Sunna ya kuomba dua kwa kutumia dua hii ya Mtume kwa ajili ya kuomba mvua.

Kufaa kuomba mvua ikate wakati mvua inapoleta madhara, na kuielekeza mvua iliyobakia katika miinuko na milima na ndani ya mabonde; kwa sababu ndio yanafaa zaidi kwa kilimo na machungo.

Inafaa kuomba kuombewa dua kutoka kwa wale wanaodhaniwa kuwa wema na wachamungu katika watu waliohai tena walioko karibu yako, na huku ndiko kuomba kupitia mtu (kutawasali) kunakofaa, ama kuomba kupitia cheo cha yeyote katika viumbe, awe hai ama maiti, hili halifai; hili halifai; kwa sababu ni miongoni mwa njia za kuingia katika ushirikina.

Sheria ya kung'ang'ania katika dua na kuirudiarudia.

Kufaa kumsemesha hatibu siku ya Ijumaa kwa haja.

Kumeonekana wazi uwezo wa Mwenyezi Mungu wa ajabu katika kuteremsha mvua na kuizuia.

Hekima ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kuomba dua kuzuia mvua ikiwa kuna madhara nakuleta ile isiyo na madhara.

Sheria ya kuomba mvua katika hotuba.

Kunyanyua mikono katika dua; kwa sababu ndani yake kuna maana ya unyenyekevu, na kutafuta maana ya kupewa ndani yake, na wamekubaliana wanachuoni juu ya kuinyanyua katika sehemu hii.

Alama miongoni mwa alama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, inayoonyesha utume wake, kwani ilijibiwa dua yake kwa wakati huo huo, katika kuleta mvua na kuiondoa.

التصنيفات

Swala ya kuomba Mvua.