usijekuacha mwisho wa kila swala kusema: Allaahumma ainni alaa dhikrika washukrika wahusni ibaadatika" Ewe Mwenyezi Mungu nisadie katika kukutaja na kukushukuru na kuzifanya vizuri ibada zako

usijekuacha mwisho wa kila swala kusema: Allaahumma ainni alaa dhikrika washukrika wahusni ibaadatika" Ewe Mwenyezi Mungu nisadie katika kukutaja na kukushukuru na kuzifanya vizuri ibada zako

Kutoka kwa Muadhi bin Jabali -radhi za Allah ziwe juu yake-: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimshika mkono wake, na akasema: "Ewe Muadhi, Wallahi hakika mimi ninakupenda", Akasema: "Ninakuusia ewe Muadhi usijekuacha mwisho wa kila swala kusema: Allaahumma ainni alaa dhikrika washukrika wahusni ibaadatika" Ewe Mwenyezi Mungu nisadie katika kukutaja na kukushukuru na kuzifanya vizuri ibada zako".

[Sahihi]

الشرح

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alishika mkono wa Muadhi radhi za Allah ziwe juu yake, na akasema kumwambia: Wallahi hakika mimi ninakupenda, na ninakuusia ewe Muadhi usijekuacha kusema mwisho wa kila swala: Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie kukutaja, katika kila kauli na kitendo kinachoniweka karibu na utiifu, "na kukushukuru" kwa kutimia neema na kuzuia mabaya, "na kuzifanya vizuri ibada zako" kwa kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa kumfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

فوائد الحديث

Sheria ya kumueleza mtu kuwa unampenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Inapendeza kuomba dua hii mwisho wa kila swala ya faradhi na ya sunna.

Katika kuomba kwa matamshi haya machache kuna mahitaji yote ya Dunia na Akhera

Katika faida za kupendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni kuusiana katika na kupeana nasaha katika mambo mema na uchamungu.

Amesema Attwayibi: Kumtaja Mwenyezi Mungu ni utangulizi wa kukunjua kifua, na kumshukuru ni njia ya kuzilinda neema, na kuzifanya vizuri ibada ni kujiweka mbali na yote yanayomshughulisha mtu na Mwenyezi Mungu Mtukufu.

التصنيفات

Adh-kaar - yasomwayo- wakati wa swala.