Je! nikujulisheni mambo ambayo yakifanyika Allah hufuta madhambi na hupandisha daraja kwa mambo hayo? wakasema: ndiyo, Ewe Mtume wa Allah, akasema: Kutawadha vizuri wakati wa baridi, na kuzidisha hatua kwenda msikitini, na kusubiria swala baada ya swala huko ndiko kuizuia nafsi katika mambo ya…

Je! nikujulisheni mambo ambayo yakifanyika Allah hufuta madhambi na hupandisha daraja kwa mambo hayo? wakasema: ndiyo, Ewe Mtume wa Allah, akasema: Kutawadha vizuri wakati wa baridi, na kuzidisha hatua kwenda msikitini, na kusubiria swala baada ya swala huko ndiko kuizuia nafsi katika mambo ya kheri.

Kutoka kwa Abi Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: amesema Mtume Muhammad Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake: ((Je! nikujulisheni mambo ambayo yakifanyika Allah hufuta madhambi na hupandisha daraja kwa mambo hayo?)) wakasema: ndiyo, Ewe Mtume wa Allah, akasema: ((Kutawadha vizuri wakati wa baridi, na kuzidisha hatua kwenda msikitini, na kusubiria swala baada ya swala huko ndiko kuizuia nafsi katika mambo ya kheri)).

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Aliwahudhurishia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- jambo maswahaba zake, na akiwa anajua ni nini watasema kumjibu, na hii ni katika uzuri wa ufundishaji wake Rehema na Amani ziwe juu yake, kuwa yeye wakati mwingine alikuwa akilileta jambo wazi, ili mtu alizingatie, na ajue ni nini kitakacholetwa kwake, Akasema: Je! nikujulisheni mambo ambayo yakifanyika Mwenyezi Mungu anafuta makosa, na ananyanyua daraja?. Wakasema: Ndivyo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, yaani tueleze kwani sisi tunatamani utueleze yale tutakayonyanyuliwa kwayo daraja na tufute makosa, Akasema: La kwanza: kutimiza udhu katika hali ambazo nafsi inakarahika, mfano siku za masika; kwasababu siku za masika maji huwa baridi, anapokamilisha mtu udhu pamoja na tabu hizi, hili linaonyesha ukamilifu wa imani, ananyanyua Mwenyezi Mungu kwa hilo daraja za mja na anamfutia madhambi. La pili: Akusudie mtu kwenda misikitini, wakati ambao ni sheria kwake kuiendea swala, na hilo linakuwa katika swala tano, hata kama msikiti utakuwa mbali. La tatu: Ni mtu awe na shauku ya swala, kila anapomaliza swala, moyo wake unakuwa umeambatana na kutaka swala nyingine anayoisubiri, Basi hili linaonyesha juu ya ukamilifu wa imani yake na mapenzi yake na shauku yake katika swala hizi tukufu. Akiwa anasubiri swala baada ya swala, basi hili ni katika yale ambayo Mwenyezi Mungu hunyanyua kwayo daraja na anafuta madhambi. Kisha akaeleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa kudumu katika twahara na swala na ibada ni kama kuifunganisha nafsi katika njia ya Mwenyezi Mungu.

التصنيفات

Ubora na fadhila za matendo mema.