إعدادات العرض
Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba uongofu na uchamungu na kujizuia na machafu nakuwa ni mwenye kutosheka
Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba uongofu na uchamungu na kujizuia na machafu nakuwa ni mwenye kutosheka
Kutoka kwa Abdallah bin Masudi radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakwamba yeye alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba uongofu na uchamungu na kujizuia na machafu nakuwa ni mwenye kutosheka".
[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt অসমীয়া Nederlands አማርኛ Hausa සිංහල ไทยالشرح
Ilikuwa miongoni mwa dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba uongofu" na njia iliyonyooka katika kuijua haki na kuifanyia kazi, "na uchamungu", kutekeleza maamrisho na kuacha makatazo, "na kujizuia na machafu" kujizuia na yale yasiyokuwa halali wala si mazuri miongoni mwa kauli au kitendo, "na kutosheka" na viumbe, kiasi ambacho asimuhitaji yeyote zaidi ya Mola wake Mlezi Aliyetakasika na kutukuka.فوائد الحديث
Utukufu wa mambo haya: Uongofu, uchamungu, na kujizuia na machafu, na kutosheka, na himizo la kujipamba nayo.
Mtume rehema na amani ziwe juu yake hamiliki juu ya nafsi yake manufaa wala madhara, na kwamba anayemiliki hayo ni Allah Mtukufu.
Anayemiliki manufaa na madhara na uongofu kwa viumbe ni Mwenyezi Mungu peke yake, si Malaika aliyekaribu wala Mtume aliyetumwa wala yeyote asiyekuwa wao.
التصنيفات
Dua zilizopokelewa toka kwa mtume.