إعدادات العرض
Atakayesema: Sub-haanallaahi wabihamdi, (Ametakasika Mwenyezi Mungu Mtukufu na sifa njema ni zake) ataoteshewa mti wa mtende peponi
Atakayesema: Sub-haanallaahi wabihamdi, (Ametakasika Mwenyezi Mungu Mtukufu na sifa njema ni zake) ataoteshewa mti wa mtende peponi
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayesema: Sub-haanallaahi wabihamdi, (Ametakasika Mwenyezi Mungu Mtukufu na sifa njema ni zake) ataoteshewa mti wa mtende peponi".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Hausa Kurdî Tiếng Việt অসমীয়া Nederlandsالشرح
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakuwa atakayesema: "Ametakasika Mwenyezi Mungu" ninamtakasa "Mtukufu" kwa dhati yake na sifa zake na vitendo vyake "na sifa njema ni zake" zikiwa zimeambatanishwa na kuegemeza sifa za ukamilifu wake Mtukufu; atasimikiwa na kupandiwa mti wa mtende katika ardhi ya Pepo kwa kila mara atakayosema.فوائد الحديث
Himizo la kukithirisha kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu, na miongoni mwake: Ni kufanya tasbihi na tahmidi (kumtukuza na kumsifu).
Pepo ni pana, na kwamba mimea yake ni tasbihi na tahmidi (Kumtuza na kumsifu), na hii ni fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na neema yake.
Umetajwa mtende pekee katika hadithi pasina miti mingine; kwa sababu ya wingi wa faida zake na uzuri wa matunda yake; na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu amepiga mfano wa muumini na imani yake ndani ya Qur'ani kwa mti huo.