إعدادات العرض
Pindi nilipopandishwa juu mbinguni, nilipita kwa watu wakiwa na kucha za shaba, wakizikwarua kwazo nyuso zao na vifua vyao
Pindi nilipopandishwa juu mbinguni, nilipita kwa watu wakiwa na kucha za shaba, wakizikwarua kwazo nyuso zao na vifua vyao
Imepokelewa kutoka kwa Anas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Pindi nilipopandishwa juu mbinguni, nilipita kwa watu wakiwa na kucha za shaba, wakizikwarua kwazo nyuso zao na vifua vyao, nikasema: Ni akina nani hao ewe Jibrili, akasema: Hawa ni wale wanaokula nyama za watu, na wanajitumbukiza katika kuvunja heshima za watu".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Bahasa Indonesia Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Français ئۇيغۇرچە Hausa Kurdî Русский Tiếng Việt Magyar ქართული සිංහල Românăالشرح
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ya kwamba yeye pindi alipopandishwa juu mbinguni usiku Israa na Miiraji (safari ya usiku na kupandishwa), alipita kwa watu wakiwa na kucha za shaba wakizikwarua na kuzichana kwazo nyuso zao na vifua vyao, akamuuliza rehema na amani ziwe juu yake Jibril amani iwe juu yake: Ni kitu gani walifanya hawa mpaka wanalipwa kwa adhabu hii? Akasema Jibril amani iwe juu yake: Hawa ni wale wanaosengenya watu, na wanazungumza vibaya kuhusu heshima zao pasina haki.فوائد الحديث
Tahadhari kubwa ya kusengenya, na amefananishwa msengenyaji na mtu anayekula nyama ya mtu.
Kutia dosari heshima za watu ni katika kuwasengenya na mfano wake ni katika madhambi makubwa.
Amesema Attwayibi: Katika kauli yake: "Wakizikwarua", Amesema: Kwa sababu kukwarua uso na kifua ni miongoni mwa sifa za wanawake wanaoomboleza kwa mayowe, basi Mwenyezi Mungu akazifanya kuwa ndio malipo ya mwenye kusengenya na kuchafua heshima za Waislamu, akionyesha kuwa hizo si katika sifa za wanaume, bali hizo ni katika sifa za wanawake wakiwa katika hali mbaya zaidi na sura mbaya mno.
Uwajibu wa kuamini ghaibu na yale yote aliyoyaeleza Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake.
التصنيفات
Kuyasema vibaya Maasi.