إعدادات العرض
Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ananyoosha mkono wake wakati wa usiku ili amsamehe mkosefu wa mchana, na ananyoosha mkono wake wakati wa mchana ili amsamehe mkosaji wa usiku, mpaka jua litakapochomoza kutoka magharibi yake
Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ananyoosha mkono wake wakati wa usiku ili amsamehe mkosefu wa mchana, na ananyoosha mkono wake wakati wa mchana ili amsamehe mkosaji wa usiku, mpaka jua litakapochomoza kutoka magharibi yake
Na kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ananyoosha mkono wake wakati wa usiku ili amsamehe mkosefu wa mchana, na ananyoosha mkono wake wakati wa mchana ili amsamehe mkosaji wa usiku, mpaka jua litakapochomoza kutoka magharibi yake."
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Hausa Kurdî Português සිංහල دری অসমীয়া Tiếng Việt አማርኛ Svenska ไทย Yorùbá Кыргызча ગુજરાતી नेपाली Română മലയാളം Nederlands Oromoo తెలుగు پښتو Soomaali Kinyarwanda Malagasy ಕನ್ನಡالشرح
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anakubali toba kutoka kwa waja wake, mja akitenda dhambi wakati wa mchana na akatubia usiku Mwenyezi Mungu hukubali toba yake, na akitenda dhambi usiku na akatubia mchana basi Mwenyezi Mungu hukubali toba yake, Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ananyoosha mkono wake kwa kuifurahia toba, na kuikubali, na mlango wa toba unabaki wazi mpaka jua lichomoze kutoka magharibi, likiashiria mwisho wa dunia, basi likichomoza mlango wa toba utafungwa.فوائد الحديث
Kukubaliwa toba kunaendelea maadamu mlango wake uko wazi, na mlango wake utafungwa wakati jua linapochomoza kutoka magharibi, na kwamba mtu atubu kabla ya msukosuko wa kifo, ambao ni roho kufika kooni.
Kutokata tamaa kwa sababu ya dhambi, kwani msamaha na rehema za Mwenyezi Mungu ni mpana, na mlango wa toba uko wazi.
Masharti ya kutubia: La kwanza: kuacha dhambi, la pili: kujuta kwa kuitenda, na la tatu: kuazimia kutorejea tena, ikiwa ni katika haki za Mwenyezi Mungu, na ikiwa inahusiana na haki za waja, basi kwa ajili ya kupokelewa toba inatakiwa kuwa haki hiyo apewe mmiliki wake au mwenye haki amsamehe.
التصنيفات
Toba