إعدادات العرض
Si katika wema kufunga safarini
Si katika wema kufunga safarini
Kutoka kwa Jaabir bin Abdillaah -radhi za Allah ziwe juu yao amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, akaona msongamano na mtu kazingirwa, akasema: "Nini hicho?", wakasema: Alikuwa kafunga swaumu, akasema: "Si katika wema kufunga safarini", na katika tamko la Muslim: "Chukuweni ruhusa ya Mwenyezi Mungu aliyokuruhusuni".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Bahasa Indonesia Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Français සිංහල ئۇيغۇرچە Hausa Português Kurdî Русский دری Македонски Tiếng Việt Magyar ქართული ไทย অসমীয়া Nederlands ਪੰਜਾਬੀالشرح
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, akaona mtu mmoja watu wamemkusanyikia na wamemzingira ili kumkinga na joto la jua na wingi wa kiu, akasema: Kapatwa na nini? Wakasema: Anaswaumu, akasema: Si katika wema kufunga safarini, Chukuweni ruhusa ya Mwenyezi Mungu aliyokuruhusuni.فوائد الحديث
Kumebainishwa wepesi wa Uislamu.
Inafaa kufunga safarini, na pia inafaa kuchukua ruhusa ya kula.
Inachukiza kufunga safarini ikiwa ataelemewa, madam hali haitomfikisha katika maangamivu.
Amesema Nawawi: Si katika wema nyinyi kufunga mkiwa safarini: Maana yake: Ikiwa swaumu itawapa tabu juu yenu na mkahofia madhara, na mlolongo wa hadithi unaashiria maana hii.
Kuwatilia umuhimu Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba zake na kuuliza kwake hali zao.
التصنيفات
Funga za watu wenye Dharura.