إعدادات العرض
Miji inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni misikiti yake, na miji inayochukiwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni masoko yake
Miji inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni misikiti yake, na miji inayochukiwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni masoko yake
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Miji inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni misikiti yake, na miji inayochukiwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni masoko yake".
[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]
الترجمة
العربية Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Hausa Kurdî Tiếng Việt Magyar ქართული සිංහල Română অসমীয়াالشرح
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa sehemu zinazopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni misikiti yake; kwa sababu ni nyumba za ibada, na zimeasisiwa kwa uchamungu, na miji inayochukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni masoko yake; kwa sababu masoko mara nyingi ndio kitovu cha ghushi na udanganyifu na riba na viapo vya uongo, na kwenda kinyume na ahadi, na kupuuza kumtaja Mwenyezi Mungu.فوائد الحديث
Utukufu wa misikiti na heshima yake; kwa sababu ni nyumba ambazo hutajwa ndani yake jina la Mwenyezi Mungu kwa wingi.
Himizo la kudumu kuwa msikitini, na wingi kwenda ndani yake, kwa kutafuta mapenzi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na radhi zake, na kupunguza kuzunguka masokoni, isipokuwa kwa haja maalumu; kwa kujiepusha kuingia katika sababu za hasira ya Mwenyezi Mungu.
Amesema Nawawi: Misikiti ni mahali pa kushuka rehema na masoko ni kinyume chake.