Amewalaani Mwenyezi Mungu Mayahudi na Wakristo, waliyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa mahali pa kusalia

Amewalaani Mwenyezi Mungu Mayahudi na Wakristo, waliyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa mahali pa kusalia

Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa katika maradhi yake ambayo hakuweza kuamka tena: "Amewalaani Mwenyezi Mungu Mayahudi na Wakristo, waliyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa mahali pa kusalia" Akasema: Na lau kama isingekuwa kauli hiyo basi lingenyanyuliwa kaburi lake, isipokuwa ilihofiwa kufanywa kuwa mahali pa kuswalia.

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anaeleza Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema akiwa katika maradhi yake ambayo yalikuwa makali na akafariki ndani yake: Mwenyezi Mungu aliwalaani Mayahudi na Wakristo, na aliwafukuza kutoka katika rehema yake; na hii ni kwa sababu wao waliyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa mahali pa kuswalia, na hii ni kwa kuyajengea au kuswali hapo au kwa kuyaelekea. Kisha akasema radhi za Allah ziwe juu yake: Na lau kama si katazo hilo na tahadhari hiyo kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na hofu ya Maswahaba kufanywa kaburi la Mtume rehema na amani ziwe juu yake kama walivyofanya Mayahudi na Wakristo kwa makaburi ya Manabii wao, basi lingedhihirishwa na kunyanyuliwa kaburi lake.

فوائد الحديث

Na huu ni mingoni mwa usia wake wa mwisho, jambo linaloonyesha umuhimu wake, na kuutilia maanani.

Katazo la msisitizo na uharamu mkubwa wa kuyafanya makaburi kuwa mahali pa kuswalia, na kuyaendea kwa ajili ya kuswali hapo swala isiyokuwa swala ya jeneza; huu ni upenyo wa kumtukuza maiti na kutufu (kuzunguka) katika kaburi lake, na kujifuta kwa nguzo zake (za kaburi), na kumuita kwa jina lake, na yote hayo ni katika ushirikina na ni katika njia zake.

Ukubwa wa kutilia umuhimu na kutilia maanani Mtume rehema na amani ziwe juu yake Tauhidi, na hofu yake juu ya kutukuzwa makaburi; kwa sababu hilo linapelekea katika ushirikina.

Mwenyezi Mungu Mtukufu alimlinda Nabii wake amani iwe juu yake, isijekufanywa shirki juu ya kaburi lake, akawapa maono Maswahaba wake na wale wanaokuja baada yao, walilinde kaburi lake lisije kunyanyuliwa.

Maswahaba kuufanyia kazi usia wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na pupa yao juu ya Tauhidi.

Katazo la kujifananisha na Mayahudi na Wakristo, na kwamba kuyajengea makaburi ni katika tamaduni zao.

Miongoni mwa aina za kuyafanya makaburi kuwa misikiti ni kuswali hapo, hata kusipojengwa msikiti.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake., Kutembelea Makaburi.