إعدادات العرض
Atakayekuwa na dhuluma yoyote ya ndugu yake kama heshima au chochote, basi na wamalizane leo hii, kabla ya wakati ambao hapatakuwa na Dinar wala Dirham
Atakayekuwa na dhuluma yoyote ya ndugu yake kama heshima au chochote, basi na wamalizane leo hii, kabla ya wakati ambao hapatakuwa na Dinar wala Dirham
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayekuwa na dhuluma yoyote ya ndugu yake kama heshima au chochote, basi na wamalizane leo hii, kabla ya wakati ambao hapatakuwa na Dinar wala Dirham, ikiwa atakuwa na amali njema basi zitachukuliwa kwake kwa kiasi cha dhuluma yake, na akiwa hana mema basi yatachukuliwa maovu ya mwenye haki na atabebeshwa yeye".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Hausa Kurdî Tiếng Việt Magyar ქართული සිංහල Română অসমীয়াالشرح
Amemuamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kutumbukia katika dhuluma ya ndugu yake Muislamu katika heshima, au mali, au damu, basi amuombe aliyemdhulumu amsamehe madamu bado yuko Duniani, kabla haijafika siku ya Kiyama, kiasi ambacho Dinar ya dhahabu wala Dirham ya fedha haitofaa kitu kwa kumlipa aliyemdhulumu ili aikomboe nafsi yake; kwani kisasi siku hiyo kitakuwa kwa matendo mema na mabaya; kiasi kwamba aliyedhulumiwa atachukua kutoka katika mema ya aliyemdhulumu kwa kiwango cha dhuluma yake alichodhulumiwa, ikiwa dhalimu hatokuwa na mema basi yatapunguzwa maovu ya aliyedhulumiwa na kubebeshwa dhalimu kwa kiwango cha dhuluma yake.فوائد الحديث
Kupupia kujiweka mbali na dhuluma na uadui.
Himizo la kufanya haraka kujiondoa katika dhima (haki za watu) katika zile alizonazo miongoni mwa haki.
Matendo mema huharibiwa na kutoweka tija yake kwa kuwadhulumu watu na kuwaudhi.
Haki za watu hazisamehi Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa kuzirejesha kwa wenye nazo.
Dinar na Dirham ni njia za kuleta manufaa katika Dunia, ama siku ya Kiyama ni matendo mema na maovu pekee.
Wamesema baadhi ya wanachuoni katika maswala ya heshima: Ikiwa aliyedhulumiwa hakujua kama alivunjiwa heshima yake, hakuna haja ya kumjulisha, mfano kama alimtukana katika kikao miongoni mwa vikao na akatubia, basi haina haja ya kumwambia, lakini anatakiwa amuombee msamaha na amuombee mazuri pia, na amtaje kwa mazuri katika kikao hicho hicho alichokuwa akimtukana ndani yake, na kwa kufanya hivyo atakuwa kajivua na hilo.
التصنيفات
Maisha ya Akhera.