Hakuna haki yoyote ya mtu muislamu anayotakiwa kuitolea usia, isipokuwa ahakikishae halali siku tatu, isipokuwa usia wake uwe umeandikwa kwake

Hakuna haki yoyote ya mtu muislamu anayotakiwa kuitolea usia, isipokuwa ahakikishae halali siku tatu, isipokuwa usia wake uwe umeandikwa kwake

Imepokelewa kutoka kwa bin Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakuna haki yoyote ya mtu muislamu anayotakiwa kuitolea usia, isipokuwa ahakikishae halali siku tatu, isipokuwa usia wake uwe umeandikwa kwake", akasema Abdallah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao: "Haukuwahi kupita usiku mmoja tangu nilipomsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akilisema hilo isipokuwa usia wangu nilikuwa nao".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuwa haitakiwi kwa muislamu anapokuwa na kitu cha kutolea usia katika haki au mali hata kama ni ndogo, alale siku tatu, isipokuwa ahakikishe usia wake umeandikwa kwake. Akasema Abdallah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao: Sikuwahi kulala hata usiku mmoja tangu nilipomsikia rehema na amani ziwe juu yake akilisema hilo isipokuwa nilikuwa nikikaa na usia wangu.

فوائد الحديث

Sheria ya kuandika usia na kuharakisha kulifanya hilo, kwa kulibainisha, na kutekeleza amri ya sheria ndani yake, na kujiandaa na kifo, na kuuonyesha na mahali pa kuutekeleza, kabla mtu hajashughulishwa na lenye kumshughulisha.

Usia: Maana yake ni ahadi, nayo ni mtu kumuahidi mtu mwingine baada ya kifo chake kupewa chochote katika mali yake, au akamuahidi mtu kumlelea watoto wake wadogo, au akamuahidi mtu katika kitu chochote katika matendo anayoyamiliki, baada ya kifo chake.

Usia unagawanyika sehemu tatu: 1- Wa Sunna, nao ni usia wa mtu katika baadhi ya mali yake, itumike katika njia za kheri, na hisani; ili zimfikie thawabu zake baada ya kifo chake. 2- Usia wa wajibu, nao ni usia wa mtu kwa haki zilizo juu yake, sawa sawa haki hizo ziwe ni za Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama zaka ambayo hakuitoa, au kafara, na mfano wake katika yale ya wajibu kwake katika msingi wa sheria, au haki hizi zikawa ni za wanadamu; kama deni, na kutekeleza amana. 3- Na Usia wa haramu: Nao ni pale atakapozidisha katika usia wake zaidi ya theluthi ya mali yake, au atakapotoa usia kwa mtu mwenye haki ya kumrithi.

Ubora wa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao, na kwenda kwake haraka kufanya mambo ya kheri, na kufuata sheria tukufu.

Amesema bin Daqiq Al-Idd: Na kuruhusu kukaa siku mbili mpaka tatu ni kwa sababu ya kuondoa uzito na ugumu.

Na mambo muhimu ni lazima yadhibitiwe kwa maandishi; kwa sababu hilo huthibitisha na kuhifadhi haki zaidi.

التصنيفات

Wasia.