إعدادات العرض
Weka mkono wako juu ya mahala panapoumia katika mwili wako, na usema: Bismillaah, (kwa jina la Mwenyezi Mungu) mara tatu, na useme mara saba: Audhubillaahi wa quduratihi min sharri maa ajidu wa uhaadhiru (Ninajikinga kwa Mwenyezi Mungu na uwezo wake kutokana na shari ya kile ninachokipata na kile…
Weka mkono wako juu ya mahala panapoumia katika mwili wako, na usema: Bismillaah, (kwa jina la Mwenyezi Mungu) mara tatu, na useme mara saba: Audhubillaahi wa quduratihi min sharri maa ajidu wa uhaadhiru (Ninajikinga kwa Mwenyezi Mungu na uwezo wake kutokana na shari ya kile ninachokipata na kile ninachokihofia)
Kutoka kwa Othman bin Abil Aswi Ath-thaqafi radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba yeye alilalamika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu maumivu anayoyapata katika mwili wake tangu aliposilimu, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: "Weka mkono wako juu ya mahala panapoumia katika mwili wako, na usema: Bismillaah, (kwa jina la Mwenyezi Mungu) mara tatu, na useme mara saba: Audhubillaahi wa quduratihi min sharri maa ajidu wa uhaadhiru (Ninajikinga kwa Mwenyezi Mungu na uwezo wake kutokana na shari ya kile ninachokipata na kile ninachokihofia)"
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt සිංහල Kurdî Português Nederlands অসমীয়া ગુજરાતી አማርኛ پښتو ไทย Hausa Română മലയാളം Deutsch नेपाली Oromooالشرح
Othman bin Abil Aswi alipata maumivu makali ambayo yalikaribia kumuua, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaenda kumtembelea, na akamfundisha dua ambayo Mwenyezi Mungu atamuondolea maradhi yaliyomfika; nayo ni aweke mkono wake juu ya mahala panapoumia, na aseme: "Bismillaah" mara tatu, kisha aseme mara saba: "Ninataka kinga" na ninajikinga na kujiweka na kujilinda (kwa Mwenyezi Mungu na kudura zake kutokana na shari za yale ninayoyapata) katika maumivu ya wakati huu (na kuyahofia) na ninahofia kutokea maumivu mengine baadaye miongoni mwa huzuni na hofu, au kuendelea kwa maradhi na yakasambaa maumivu yake katika mwili.فوائد الحديث
Sunna ya mtu kujifanyia kisomo cha ruqya yeye mwenyewe kama ilivyokuja katika hadithi.
Malalamiko -pasina kuchukizwa na hali wala kupingana na Kadari- hakupingani na kutawakali na subira.
Dua ni miongoni mwa kuchukua sababu, na ndio maana ni lazima kushikamana na matamshi yake na idadi yake.
Dua hii inasomwa kwa maumivu ya kila kiungo.
Kuweka mkono juu ya mahala palipo na maumivu wakati wa kusoma dua hii.
التصنيفات
Ruq'ya ya Kisheria.