Atakayesema wakati anamsikia muadhini: Ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika nakuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake, nimeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ni Mola wangu na Muhammadi kuwa ni Mtume na Uislamu kuwa ni dini,…

Atakayesema wakati anamsikia muadhini: Ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika nakuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake, nimeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ni Mola wangu na Muhammadi kuwa ni Mtume na Uislamu kuwa ni dini, atasamehewa dhambi zake

Kutoka kwa Sa'd Bin Abi Waqaas Allah amridhie kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayesema wakati anamsikia muadhini: Ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika nakuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake, nimeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ni Mola wangu na Muhammadi kuwa ni Mtume na Uislamu kuwa ni dini, atasamehewa dhambi zake".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema wakati akimsikia muadhini "Ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika wake", Yaani: Nina kiri na kukubali na ninatoa habari kuwa hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kila mwenye kuabudiwa kinyume na yeye ni batili, "Na kuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake" Yaani: Yeye ni mja wala haabudiwi, na ni Mjumbe wake haongopi, "Nimeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi" Yaani: Kwa ulezi wake na uungu wake na majina yake na sifa zake, "Na Muhammadi kuwa ni Mtume" Yaani: Kwa yote aliyotumwa kwayo, na akatufikishia, "Na Uislamu" Yaani: Kwa hukumu zote za Uislamu ikiwemo maamrisho na makatazo, "Dini" Yaani: Kwa itikadi na kutii, "Atasamehewa dhambi zake" Yaani: Katika dhambi ndogo.

فوائد الحديث

Kuirudia rudia dua hii wakati wa kusikia adhana ni miongoni mwa mambo yanayofuta madhambi.

التصنيفات

Adhana na Iqama.