إعدادات العرض
Hakuwahi kupewa hiyari Mtume rehema na amani ziwe juu yake baina ya mambo mawili hata siku moja isipokuwa atachukua jepesi lake, madamu si dhambi, ikiwa itakuwa ni dhambi, basi hujiwekanalo mbali kuliko watu wote
Hakuwahi kupewa hiyari Mtume rehema na amani ziwe juu yake baina ya mambo mawili hata siku moja isipokuwa atachukua jepesi lake, madamu si dhambi, ikiwa itakuwa ni dhambi, basi hujiwekanalo mbali kuliko watu wote
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Hakuwahi kupewa hiyari Mtume rehema na amani ziwe juu yake baina ya mambo mawili hata siku moja isipokuwa atachukua jepesi lake, madamu si dhambi, ikiwa itakuwa ni dhambi, basi hujiwekanalo mbali kuliko watu wote, na hakuwahi kulipiza kisasi Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- katika kitu ambacho kina masilahi yake binafsi katu, isipokuwa kama zitavunjwa sheria za Mwenyezi Mungu, hapo hulipiza kisasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Hausa Kurdî Português සිංහල Русский অসমীয়া Српски Tiếng Việt ગુજરાતીالشرح
Ameeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake baadhi ya tabia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na miongoni mwa zile alizozieleza: Nikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakuwahi kupewa hiyari baina ya mambo mawili isipokuwa alichukua jepesi zaidi kati ya hayo, madamu hilo jepesi halipelekei katika madhambi, basi alikuwa akijiweka mbali zaidi kuliko watu wote, na hapo anachagua gumu zaidi. Hakuwahi kulipiza kisasi rehema na amani ziwe juu yake kwa ajili ya nafsi yake binafsi, bali alikuwa akisamehe na kufuta katika haki yake isipokuwa yakivunjwa maharamisho ya Mwenyezi Mungu hapo analipiza kisasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na alikuwa ni mtu mwenye hasira kuliko watu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.فوائد الحديث
Sunna ya kuchukua jepesi katika mambo madamu hakuna maasi ndani yake.
Wepesi wa Uislamu.
Sheria ya kukasirika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika upole na subira na kutekeleza haki katika kusimamisha sheria na mipaka ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Amesema bin Hajari: Na hapa kuna kuacha kuchukua jambo gumu, na kutosheka na jepesi, na kuacha kung'ang'ania katika yale yasiyokuwa ya dharura.
Himizo la kusamehe isipokuwa katika haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu.