Wapigeni vita washirikina kwa mali zenu na nafsi zenu na ndimi zenu

Wapigeni vita washirikina kwa mali zenu na nafsi zenu na ndimi zenu

Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Wapigeni vita washirikina kwa mali zenu na nafsi zenu na ndimi zenu".

[Sahihi]

الشرح

Aliamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwapiga vita makafiri, na kutumia juhudi katika kukabiliana nao kwa kila nyenzo kwa kadri iwezekanavyo, ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu, na miongoni mwake: Kwanza: Kutoa mali katika kuwapiga vita; ikiwemo kununua silaha, na kutoa mahitaji kwa wapiganaji, na mfano wake. Pili: Kutoka kwa nafsi na mwili ili kukabiliana nao na kuwazuia. Tatu: Kwa kuwalingania waingie katika dini hii kwa ulimi, na kuwasimamishia hoja juu yao, na kuwakemea na kuwajibu hoja zao.

فوائد الحديث

Himizo la kupigana Jihadi na washirikina kwa nafsi na mali na ulimi; kila mmoja kulingana na uwezo wake, nakuwa Jihadi haishii katika kukabiliana nao kwa nafsi pekee.

Amri ya Jihadi ni ya wajibu, na inaweza kuwa wajibu kwa kila mtu, na inaweza kuwa wajibu kwa watu baadhi.

Mwenyezi Mungu aliweka sheria ya Jihadi kwa mambo mengi, miongoni mwake: La kwanza: Kupambana na ushirikina na washirikina; kwa sababu Mwenyezi Mungu haukubali ushirikina milele, la pili: Kuondoa vikwazo vinavyojitokeza katika njia ya ujumbe wa Mwenyezi Mungu, la tatu: Kuihami itikadi sahihi dhidi ya yote yaliyokinyume nayo, la nne: Kuwalinda waislamu na nchi zao na mali zao.

التصنيفات

Hukumu ya Jihadi.