Umekwisha pokea malipo yako kutokana na mema uliyoyatanguliza

Umekwisha pokea malipo yako kutokana na mema uliyoyatanguliza

Imepokelewa kutoka kwa Hakiim Bin Hizaam -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni upi mtazamo wako katika mambo ambayo nilikuwa nikifanya ibada kupitia mambo hayo kabla ya kuwa muislamu, miongoni mwa sadaka, au kumwacha huru mtumwa, au kuunganisha udugu, je katika mambo hayo kuna malipo? Basi akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: " Umekwisha pokea malipo yako kutokana na mema uliyoyatanguliza".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kafiri anaposilimu hulipwa kwa mema aliyokuwa akiyafanya kabla ya kusilimu miongoni mwa sadaka au kuacha huru mtumwa au kuunganisha udugu.

فوائد الحديث

Kwa hakika mema aliyofanya kafiri hapa Duniani, hatolipwa kule Akhera, ikiwa atakufa akiwa kwenye ukafiri wake.

التصنيفات

Uislamu