إعدادات العرض
Nieleze ndani ya Uislamu kauli ambayo sitomuuliza yeyote zaidi yako, akasema: "Sema: Nimemuamini Mwenyezi Mungu, kisha kuwa na msimamo
Nieleze ndani ya Uislamu kauli ambayo sitomuuliza yeyote zaidi yako, akasema: "Sema: Nimemuamini Mwenyezi Mungu, kisha kuwa na msimamo
Kutoka kwa Sufiani bin Abdillah Al-Thaqafi Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Nieleze ndani ya Uislamu kauli ambayo sitomuuliza yeyote zaidi yako, akasema: "Sema: Nimemuamini Mwenyezi Mungu, kisha kuwa na msimamo".
الترجمة
العربية English မြန်မာ Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá اردو Bahasa Indonesia ئۇيغۇرچە Türkçe සිංහල हिन्दी Tiếng Việt Hausa ไทย پښتو অসমীয়া دری Кыргызча or नेपाली Malagasy Română Kinyarwanda বাংলা తెలుగు Bosanski Kurdî Lietuvių Oromoo മലയാളം Nederlands Soomaali Shqip Српски Deutsch Українська ಕನ್ನಡ Wolof Mooreالشرح
Swahaba Sufiani bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake alimuomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amfundishe kauli iliyokusanya maana nzima ya Uislamu ili ashikamane nayo na wala hatomuuliza yeyote zaidi yake? Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Sema: Nimempwekesha Mwenyezi Mungu, na nimemuamini kuwa yeye ndiye Mola wangu na Mungu wangu na Muumba wangu na muabudiwa wangu wa haki aisye na mshirika wake, kisha awe mtiifu katika sheria za Mwenyezi Mungu kwa kutekeleza faradhi za Mwenyezi Mungu na kuacha maharamisho ya Mwenyezi Mungu na adumu katika hilo.فوائد الحديث
Msingi wa Dini ni kumuamini Mwenyezi Mungu kwa Ulezi wake na uungu wake na majina yake na sifa zake.
Umuhimu wa kuwa na msimamo baada ya kuamini, na kudumu na ibada na kuthubutu juu ya hilo.
Imani ni sharti la kukubaliwa matendo.
Kumuamini Mwenyezi Mungu kunakusanya yote yanayopaswa kuitakidi miongoni mwa itikadi za imani na misingi yake, na yanayofuata hilo miongoni mwa amali za moyo, na kutii na kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kwa siri na kwa wazi.
Msimamo ni kubaki katika njia, kwa kutekeleza wajibu na kuacha makatazo.