Ataikamata Mwenyezi Mungu ardhi, na ataikunja mbingu kwa mkono wake wa kulia kisha atasema: Mimi ndiye Mfalme; wako wapi wafalme wa ardhi?

Ataikamata Mwenyezi Mungu ardhi, na ataikunja mbingu kwa mkono wake wa kulia kisha atasema: Mimi ndiye Mfalme; wako wapi wafalme wa ardhi?

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Ataikamata Mwenyezi Mungu ardhi, na ataikunja mbingu kwa mkono wake wa kulia kisha atasema: Mimi ndiye Mfalme; wako wapi wafalme wa ardhi?"

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu Mtukufu ataikamata Ardhi na kuikusanya, na ataikunja Mbingu kwa mkono wake wa kulia na aikunjekunje na aiondoe na aimalize, kisha asema: Mimi ndiye Mfalme, wako wapi wafalme wa Ardhini?!

فوائد الحديث

Ukumbusho wa kuwa Ufalme wa Mwenyezi Mungu ndio wenye kubakia, na Ufalme wa asiyekuwa yeye ni wenye kuondoka.

Utukufu wa Mwenyezi Mungu na Ukubwa wa kudura zake na mamlaka yake na ukamilifu wa Ufalme wake.

التصنيفات

Kumuamini Allah mwenye nguvu alie tukuka, Kuamini siku ya mwisho, Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake.