إعدادات العرض
Yale niliyokukatazeni basi yaepukeni, na yale niliyokuamrisheni basi fanyeni katika hayo kadiri muwezavyo
Yale niliyokukatazeni basi yaepukeni, na yale niliyokuamrisheni basi fanyeni katika hayo kadiri muwezavyo
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira Abdul-Rahman bin Swakhar -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Yale niliyokukatazeni basi yaepukeni, na yale niliyokuamrisheni basi fanyeni katika hayo kadiri muwezavyo, na hakika waliangamia wale waliokuwa kabla yenu, kwa kukithiri maswali yao, na kuhitilafiana kwao na Manabii wao".
الترجمة
العربية Español አማርኛ English اردو Indonesia বাংলা Français Türkçe Русский Bosanski සිංහල हिन्दी 中文 فارسی Tiếng Việt Tagalog Kurdî Hausa Português മലയാളം తెలుగు தமிழ் ไทย Deutsch پښتو অসমীয়া Shqip Nederlands ગુજરાતી Кыргызча नेपाली Lietuvių دری Српски тоҷикӣ Kinyarwanda Română Magyar Čeština Moore Malagasy Oromoo ಕನ್ನಡ Wolof Azərbaycan O‘zbek Українська ქართული Македонски ភាសាខ្មែរ ਪੰਜਾਬੀ मराठी Kirundi Kurmancî Bahasa Melayuالشرح
Ametubainishia sisi Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuwa atakapotukataza kitu basi ni wajibu juu yetu kukiacha pasina kubagua, na atakapotuamrisha kwa chochote basi ni juu yetu kukifanya kile tunachokiweza. Kisha akatutahadharisha ili tusije kuwa kama baadhi ya umma zilizopita pindi walipokithirisha maswali juu ya Manabii wao ikiwa ni pamoja na kwenda kinyume nao, basi Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa aina mbali mbali za maangamivu na uharibifu, tunatakiwa tusiwe mfano wao ili tusiangamie kama walivyoangamia.فوائد الحديث
Hadithi ni kanuni katika kubainisha kuwa la wajibu ni kutekeleza amri na kujiepusha na makatazo.
Katazo halikuruhusu kufanya chochote katika hayo, lakini amri imewekwa sharti la uwezo; kwa sababu kuacha ni jambo liko ndani ya uwezo na kufanya kunahitaji uwezo wa kuleta kitendo kilichoamrishwa.
Katazo la kuuliza maswali mengi Wanachuoni wamegawanya kuuliza katika sehemu mbili: Moja wapo: Ni maswali yanayokuwa katika mfumo wa kujifunza yale anayoyahitajia mtu kuhusiana na mambo ya dini, hili limeamrishwa, na miongoni mwa aina hii ni maswali ya Maswahaba, na aina ya pili: Ni maswali yanayokuwa katika sura ya kiburi na kujikalifisha, na hii ndiyo iliyoharamishwa.
Tahadhari kwa Umma huu dhidi ya kumpinga Nabii wake, kama ilivyotokea katika Umma zilizokuwa kabla yake.
Makatazo yanakusanya kidogo na mengi; kwa sababu haiwezekani kuyaepuka ila kwa kuyaepuka kidogo yake na mengi yake, kwa mfano: Ametukataza riba hii inakusanya ndogo yake na kubwa yake.
Kuacha sababu zinazopelekea katika haramu; kwa sababu hilo ni miongoni mwa maana za kuepeuka.
Haitakiwi kwa mtu atakaposikia amri ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake aseme: Je ni wajibu au ni sunna?, bali anawajibika kwenda mbio kutekeleza; kwa kauli yake: "Yafanyeni katika hayo kadiri muwezavyo".
Wingi wa maswali ni sababu ya kuangamia hasa hasa katika mambo ambayo haiwezekani kuyafikia, mfano kama mambo ya ghaibu, na namna ya hali ya siku ya Kiyama, usizidishe maswali ndani yake utaangamia, na ukawa ni king'ang'anizi na mtafuta mambo kwa undani.
