إعدادات العرض
Hawezi kuwa na imani mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake anachokipenda yeye katika nafsi yake
Hawezi kuwa na imani mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake anachokipenda yeye katika nafsi yake
Kutoka kwa Abuu Hamza Anas bin Maaliki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake mtumishi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hawezi kuwa na imani mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake anachokipenda yeye katika nafsi yake".
الترجمة
العربية Español አማርኛ English اردو Indonesia বাংলা Français Türkçe Русский Bosanski සිංහල हिन्दी 中文 فارسی Tiếng Việt Tagalog Kurdî Hausa Português മലയാളം తెలుగు தமிழ் မြန်မာ ไทย Deutsch 日本語 پښتو অসমীয়া Shqip Svenska Nederlands ગુજરાતી Кыргызча नेपाली Lietuvių دری Српски тоҷикӣ Kinyarwanda Română Magyar Čeština Moore Malagasy Oromoo ಕನ್ನಡ Wolof Azərbaycan O‘zbek Українська ქართული Македонски ភាសាខ្មែរ ਪੰਜਾਬੀ मराठी Kirundi Kurmancî Bahasa Melayu Yaoالشرح
Amebainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa imani kamili ya Muislamu yeyote haikamiliki mpaka ampendelee nduguye anachokipenda yeye, katika matendo mema, na aina mbalimbali za wema katika dini na dunia, na achukie kwake kinachochukiwa na nafsi yake, na ikiwa ataona kwa ndugu yake Muislamu kuna upungufu katika dini yake, basi ajitahidi kurekebisha, na akiona kuna jambo la kheri basi amtie moyo na amsaidie, na amnasihi katika dini yake au mambo ya dunia yake.فوائد الحديث
Ulazima wa mtu kumpendelea ndugu yake kile anachokipenda kwa nafsi yake. Kwa sababu kukanushwa imani kwa mtu ambaye hampendelei ndugu yake kile anachopenda yeye mwenyewe kunaonyesha ulazima wa hilo.
Udugu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu uko juu zaidi kuliko udugu wa nasaba (ukoo), kwani haki yake ni wajibu.
Katazo la maneno na vitendo vyote vinavyopingana na upendo huu, kama vile udanganyifu, kusengenya, husuda, na uadui dhidi ya mtu, au mali yake, au heshima yake.
Kutumia baadhi ya maneno yanayotia hamasa ya kufanya matendo; kwa kauli yake "Kwa ndugu yake".
Amesema Al-Kirmani, Mwenyezi Mungu amrehemu: Pia ni sehemu ya imani kuchukia kwa ndugu yake uovu anaouchukia kwa nafsi yake, na hili (Mtume) hakulitaja, kwa sababu kukipenda kitu kunalazimu kuchukia kinyume chake, hivyo kuacha kutolisema hilo inatosha.
