Wakati wakazi wa Peponi watakapoingia Peponi, Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, atasema: "Je, mnataka kitu chochote niwazidishie?

Wakati wakazi wa Peponi watakapoingia Peponi, Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, atasema: "Je, mnataka kitu chochote niwazidishie?

Na imesimuliwa kutoka kwa Suhaib Mwenyezi Mungu amridhie, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Wakati wakazi wa Peponi watakapoingia Peponi, Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, atasema: "Je, mnataka kitu chochote niwazidishie?" Watasema: "Je, hukuziangaza nyuso zetu? Je, hukutuingiza Peponi, na ukatuokoa kutokana na Moto?" Kisha (Mwenyezi Mungu) atainua pazia, basi, hawatapewa kitu chochote kinachopendwa zaidi kwao kuliko kumwangalia Mola wao Mlezi Mwenye Nguvu, Mtukufu."

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa watakapoingia watu wa peponi peponi, Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka atasema kuwaambia: Je, mnahitaji chochote nikuongezeeni? Watasema watu wa peponi wote kwa pamoja: Kwani hujazitia nuru nyuso zetu, kwani hujatuingiza peponi, na ukatuokoa na moto? Hapo, Mwenyezi Mungu Mtukufu ataondoa pazia na kulinyanyua; na pazia lake ni nuru, watajikuta hawajapewa kitu wanachokipenda zaidi kwao kuliko kumtazama Mola wao Mlezi Aliyetakasika na kutukuka.

فوائد الحديث

Kufunuliwa pazia kwa watu wa peponi, watamuona Mola wao, na ama makafiri; watazuiliwa na hilo.

Neema kubwa zaidi ya peponi ni waumini kumuona Mola wao Mlezi.

Watu wa peponi wote vyovyote vile zitakavyotofautiana daraja zao watamuona Mola wao Mlezi Aliyetakasika na kutukuka.

Fadhila za Mwenyezi Mungu kwa waumini kwa kuwaingiza peponi.

Umuhimu wa kwenda haraka peponi kwa kutenda amali njema na kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake.

التصنيفات

Sifa za pepo na moto.