إعدادات العرض
Hakika shetani alishakata tamaa kuabudiwa na wenye kuswali katika kisiwa cha Arab, Lakini yuko katika kuwachochea baina yao
Hakika shetani alishakata tamaa kuabudiwa na wenye kuswali katika kisiwa cha Arab, Lakini yuko katika kuwachochea baina yao
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika shetani alishakata tamaa kuabudiwa na wenye kuswali katika kisiwa cha Arab, Lakini yuko katika kuwachochea baina yao".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt සිංහල Hausa Kurdî Português தமிழ் Nederlands অসমীয়া ગુજરાતી አማርኛ پښتو ไทย മലയാളം नेपालीالشرح
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Ibilisi amekwishakata tamaa waumini wenye kuswali kurudi kuabudu na kusujudia masanamu katika kisiwa Arab, lakini bado anatamaa, na bado nguvu zake na juhudi zake na harakati zake ziko katika kuwachochea baina yao kwa ugomvi na chuki na vita na fitina na mfano wa hayo.فوائد الحديث
Kumuabudu Shetani ni kuabudu sanamu, kwa sababu yeye ndiye muamrishaji na mshawishi wa hilo, kwa dalili ya kauli yake Mtukufu kuhusu Nabii Ibrahim -amani iwe juu yake- (aliposema): "Ewe baba yangu usimuabudu Shetani...."
Shetani anakwenda mbio katika kuchochea ugomvi na chuki na vita na fitina baina ya waislamu.
Miongoni mwa faida za swala katika Uislamu nikuwa inalinda mapenzi kati ya waislamu, na ikayatia nguvu mahusiano ya kiudugu baina yao.
Swala ndiyo nembo kubwa ya dini baada ya shahada mbili, na ndio maana wameitwa waislamu wanaoswali.
Kisiwa Arab kina mambo maalumu yasiyokuwepo katika miji mingine.
Ikiwa kutasema kuwa, mbona kumetokea katika baadhi ya Kisiwa Arab ibada za masanamu, hali yakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anasema: "Hakika Shetani amekwishakata tamaa ya kuabudiwa na wenye kuswali...", hii ni taarifa ya yale yaliyotokea katika nafsi ya Shetani katika kukata tamaa baada ya kuona ufunguzi wa miji mbali mbali, na watu kuingia ndani ya dini ya Mwenyezi Mungu makundi kwa makundi, hadithi imeeleza dhana ya Shetani na kutokea kwake, kisha uhalisia ukawa kinyume na matarajio kwa hekima aliyoitaka Mwenyezi Mungu Mtukufu.
التصنيفات
Tabia mbovu.