Kuoga siku ya Ijumaa ni wajibu kwa kila aliyebaleghe, na apige mswaki, na aguse marashi ikiwa atapata

Kuoga siku ya Ijumaa ni wajibu kwa kila aliyebaleghe, na apige mswaki, na aguse marashi ikiwa atapata

Kutoka kwa Amri Bin Suleim Al-Answari amesema: Ninamshuhudilia Abuu Saidi kuwa alisema: Ninamshuhudilia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuwa alisema: "Kuoga siku ya Ijumaa ni wajibu kwa kila aliyebaleghe, na apige mswaki, na aguse marashi ikiwa atapata".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Amebainisha Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kuoga siku ya Ijumaa kumetiliwa mkazo ni sawa na wajibu upande wa kila aliyebalehe katika waislamu waliowajibikiwa na Ijumaa, Na asafishe meno yake kwa mswaki na mfano wake, na ajitie manukato kwa harufu yoyote nzuri ya uturi.

فوائد الحديث

Kumetiwa mkazo kuoga siku ya Ijumaa kwa kila mwanaume wa kiislamu aliyebaleghe.

Usafi na kuondoa harufu mbaya ni jambo linalotakiwa na ni sheria kwa muislamu.

Kuitukuza siku ya Ijumaa, na kujiandaa kwa ajili yake.

Mkazo wa kutumia mswaki siku ya Ijumaa.

Sunna ya kujipaka manukato kwa harufu yoyote nzuri kabla ya kwenda katika swala ya Ijumaa.

Mwanamke akitoka nyumbani kwake kwa ajili swala ua kinginecho, haifai kwake kujitia manukato; kwa sababu mafundisho ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yamekataza hilo.

Anayejiotea ni mtu aliyebaleghe, na kubaleghe hutokea kwa alama mbali mbali, tatu kati yake wanashirikiana wanaume na wanawake nazo ni: Ya kwanza: Kukamilisha miaka kumi na tano. Ya pili: Zikiota nywele pembezoni mwa tupu. Ya tatu: Kushusha manii kwa kujiotea au kwa matamanio au bila matamanio. Ama alama ya nne: Hii inamuhusu mwanamke, nayo ni: Hedhi, mwanamke akipata hedhi, anakuwa tayari kabaleghe.

التصنيفات

Hukumu wa Swala ya Ijumaa., Hukumu wa Swala ya Ijumaa.