إعدادات العرض
Atakapopata shaka mmoja wenu katika swala yake, akawa hajui kaswali rakaa ngapi tatu au nne? Basi aachane na shaka na ajenge yakini (uhakika), kisha atasujudu sijida mbili kabla hajatoa salamu
Atakapopata shaka mmoja wenu katika swala yake, akawa hajui kaswali rakaa ngapi tatu au nne? Basi aachane na shaka na ajenge yakini (uhakika), kisha atasujudu sijida mbili kabla hajatoa salamu
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khuduriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakapopata shaka mmoja wenu katika swala yake, akawa hajui kaswali rakaa ngapi tatu au nne? Basi aachane na shaka na ajenge yakini (uhakika), kisha atasujudu sijida mbili kabla hajatoa salamu, ikiwa atakuwa kaswali rakaa tano basi zitamtetea katika swala yake, na kama aliswali kukamilisha nne; basi hiyo itakuwa ni kumvunja moyo shetani."
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو हिन्दी 中文 Kurdî Português دری অসমীয়া Tiếng Việt አማርኛ Svenska ไทย Yorùbá Кыргызча ગુજરાતી Hausa नेपाली Română മലയാളം Nederlands Oromoo සිංහල پښتو తెలుగు Soomaali Kinyarwanda Malagasy ಕನ್ನಡ Српски Moore ქართულიالشرح
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ikiwa mwenye kuswali atasita katika swala yake na akashindwa kujua ameswali rakaa ngapi, tatu au nne? Hebu aondoe idadi iliyozidi yenye shaka na asiihesabu; tatu ndiyo ana uhakika nazo, basi ataswali rakaa ya nne, kisha atasujudu sijida mbili kabla ya kutoa salamu. Ikiwa aliswali nne kweli; basi zitakuwa tano kwa kuongeza rakaa moja, na sijida mbili za kusahau zitakuwa ni mbadala wa rakaa moja, basi idadi itakuwa ni shufa si witiri, na ikiwa kaswali rakaa nne kwa rakaa iliyozidi; basi atakuwa katekeleza wajibu wake pasina kuongeza wala kupunguza. Sijida mbili za kusahau zilikuwa ni kumdhalilisha Shetani na kumshinda, na kumrudisha akiwa kafedheheka, na kashindwa kufikia lengo lake; Kwa sababu alimvurugia swala yake, na akataka kuiharibu, na ikakamilika swala ya mwanadamu alipotekeleza amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ya kusujudu, sijida ambayo Ibilisi aliasi, alipokataa kumtii Mwenyezi Mungu kwa kumsujudia Adamu.فوائد الحديث
Mwenye kuswali akiitilia shaka swala yake na akawa hakupata ufumbuzi wa moja kati ya mambo mawili, basi aondoe shaka na afanyie kazi uhakika, ambao ni uchache, basi atatimiza swala yake na atasujudu kwa ajili ya kusahau kabla hajatoa salamu kisha atatoa salamu.
Sijida hizi mbili ni njia ya kurekebisha swala, na kumrudisha Shetani katika hali ya udhalili na unyonge, mbali na alichotaka.
Shaka iliyoko katika Hadithi ni kusitasita bila ya kupata majibu, hivyo ikipatikana dhana na akapata majibu basi atafanyia kazi dhana yake.
Himizo la kupambana na wasi wasi na kuuzuia kwa kutekeleza amri ya sheria.