إعدادات العرض
Madhambi makubwa: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kuwaasi wazazi wawili, na kuuwa nafsi, na kiapo cha uongo
Madhambi makubwa: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kuwaasi wazazi wawili, na kuuwa nafsi, na kiapo cha uongo
Imepokewa kutoka kwa Abdillah Ibn Amri bin Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Madhambi makubwa: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kuwaasi wazazi wawili, na kuuwa nafsi, na kiapo cha uongo".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Tiếng Việt Kurdî Hausa Português മലയാളം తెలుగు မြန်မာ Deutsch 日本語 پښتو অসমীয়া Shqip Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands ئۇيغۇرچە සිංහල தமிழ் ไทย دری Кыргызча Lietuvių Kinyarwanda नेपाली Malagasy Italiano or ಕನ್ನಡ Oromoo Română Soomaali Српски Wolof Moore Українська Azərbaycan ქართული Magyarالشرح
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- madhambi makubwa, nayo ni yale aliyokemewa mfanyaji wake kwa kemeo la adhabu kali duniani au Akhera. La kwanza lake "Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu": Nalo ni kukielekeza chochote katika aina za ibada kwa asiyekuwa Allah, na kumfanya kuwa sawa na Allah asiyekuwa Allah katika yale ambayo ni maalumu kwa Allah katika uungu wake na uumbaji wake na majina yake na sifa zake. Na la pili lake "Ni kuwaasi wazazi wawili": Nalo ni kila linalopelekea kuwaudhi wazazi wawili sawa sawa iwe kauli au kitendo, na kuacha kuwatendea wema. Na la tatu lake: "Ni kuua nafsi": Bila hatia, kama kuuwa kwa dhulma na uadui. Na la nne lake "Kiapo cha uongo": Nako ni kuapia uongo huku ukijua kuwa ni uongo, umeitwa hivyo; Kwa sababu humzamisha mfanyaji wake katika madhambi au motoni.فوائد الحديث
Kiapo cha uongo hakina kafara; kwa ubaya wa hatari yake, bali kinatoba.
Kuishia kutaja madhambi makubwa haya manne katika hadithi ni kwa sababu ya ukubwa wa dhambi zake, na si kwa kudhibiti idadi yake.
Madhambi yanagawanyika makubwa na madogo, na dhambi kubwa ni: Kila dhambi lenye adhabu duniani, kama kusimamishiwa sheria na laana, au ahadi ya adhabu ya Akhera, kama ahadi ya adhabu ya moto, pia madhambi makubwa yana daraja, baadhi yake ni mazito kuliko mengine katika uharamu, na madhambi madogo nayo ni yale yasiyokuwa makubwa.
التصنيفات
Kuyasema vibaya Maasi.