Sikumuona Mtume -rehema amani ziwe juu yake- katu akipitiliza kucheka mpaka kionekane Kilimi ndani ya mdomo wake, bali alikuwa akitabasamu

Sikumuona Mtume -rehema amani ziwe juu yake- katu akipitiliza kucheka mpaka kionekane Kilimi ndani ya mdomo wake, bali alikuwa akitabasamu

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, amesema: Sikumuona Mtume -rehema amani ziwe juu yake- katu akipitiliza kucheka mpaka kionekane Kilimi ndani ya mdomo wake, bali alikuwa akitabasamu.

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Alieleza Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Mtume rehema amani ziwe juu yake alikuwa hapitilizi kucheka mpaka kionekane kilimi chake, nacho ni kinyama kinachoning'inia juu ya koo, bali alikuwa akitabasam.

فوائد الحديث

Kulikuwa kucheka kwa Mtume rehema amani ziwe juu yake ni kutabasam anaporidhia au kufurahishwa na jambo.

Amesema bin Hajari: Sikuwahi kumuona akipitiliza katika kucheka kiasi cha kucheka kicheko kamili kwa kujiachia mzima mzima kwa kicheko.

Kukithirisha kucheka na kunyanyua sauti kwa kujikohoza hii si miongoni mwa sifa za watu wema.

Kukithirisha kucheka kunaondoa haiba ya mtu na heshima yake mbele ya ndugu zake.

التصنيفات

Kucheka kwake Mtume Rehma na za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amani: