إعدادات العرض
Laiti nisingeliogopea uzito kwa waumini -au kwa umma wangu-; ningeliwaamrisha kupiga mswaki kila wakati wa swala
Laiti nisingeliogopea uzito kwa waumini -au kwa umma wangu-; ningeliwaamrisha kupiga mswaki kila wakati wa swala
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Laiti nisingeliogopea uzito kwa waumini -au kwa umma wangu-; ningeliwaamrisha kupiga mswaki kila wakati wa swala".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Hausa Português Kurdî සිංහල Nederlands Tiếng Việt ગુજરાતી অসমীয়া አማርኛ پښتو ไทยالشرح
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake lau kama si hofu ya kuwatia tabu waumini katika umma wake basi angeliwawajibishia juu yao kutumia mswaki kwa kila swala.فوائد الحديث
Huruma ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa umma wake, na kuchelea kwake kuwatia tabu juu yao.
Asili katika amri za Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni ulazima, isipokuwa itakapokuja dalili kuwa ni sunna.
Sunna ya kupiga mswaki na fadhila zake wakati wa kila swala.
Amesema bin Daqiq Al-Idd: Hekima ya kufanywa sunna ya mswaki wakati wa kusimama katika swala ni kwa sababu ni mtu ajikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, ikawa ni lazima awe katika hali ya ukamilifu na usafi na kuonyesha heshima ya ibada.
Ujumla wa hadithi unajumuisha kupiga mswaki kwa mfungaji hata ikiwa baada ya kupinduka jua, kama swala mbili za Adhuhuri na Lasiri.
التصنيفات
Mambo ya Mtume.