Wanaendelea watu kuwa katika kheri kwa muda wote watakaofanya haraka kufuturu

Wanaendelea watu kuwa katika kheri kwa muda wote watakaofanya haraka kufuturu

Kutoka kwa Sahli bin Sa'ad radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Wanaendelea watu kuwa katika kheri kwa muda wote watakaofanya haraka kufuturu".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa watu wataendelea kuwa katika kheri kwa muda wote watakaofanya haraka kufuturu ndani ya Ramadhani baada kuhakiki kuzama kwa Jua; na hii ni kwa sababu ya kutekeleza sunna, na kusimama katika mpaka wake.

فوائد الحديث

Amesema Nawawi: Hapa kuna himizo la kuwahisha kufuturu baada ya kuhakikisha kuzama kwa Jua, na maana yake nikuwa jambo la umma litaendelea kuwa katika nidhamu nao wakiwa katika kheri madam wanadumu na sunna hii, na wakichelewesha hiyo itakuwa ni alama ya kuharibikiwa wanakoangukia.

Kubakia kwa kheri kwa watu ni kwa sababu ya kufuata kwao sunna, na kuharibika kwa mambo kunahusiana na kubadilishwa kwa sunna.

Kwenda kinyume na Mayahudi na wakristo na watu wa bid'a, kwani wao huchelewesha kufuturu.

Amesema bin Hajari: Hapa kumebainishwa sababu katika hilo, amesema Muhallab: Na hekima katika hilo ili mchana usiongezwe kuwa mrefu kwa kuchukua sehemu ya usiku, na ni kwa sababu mchana ndio mzuri kwa kufunga na unamtia nguvu kwake ya kufunga, na wamekubaliana wanachuoni kuwa mahala pa hilo ni pale kutakapothibitika kuzama kwa Jua kwa kuliona au kupewa habari na waadilifu wawili, na hata muadilifu mmoja katika kauli yenye nguvu zaidi anatosha.

Amesema bin Hajari: Angalizo: Miongoni mwa bid'a mbaya ni yale yaliyozushwa katika zama hizi kwa kutoa adhana ya pili kabla ya Alfajiri kwa takribani saa nzima ndani ya Ramadhani, na kuzima taa ambazo zimewekwa kuwa ni alama ya kuharamisha kula na kunywa kwa yule mwenye kutaka kufunga, kwa madai kutoka kwa yule aliyezusha hilo kuwa wanachukua tahadhari katika ibada, na hawalifahamu hilo ila watu wachache, na liliwatia ujasiri hilo mpaka wakafikia kutoadhini ila baada ya kuzama Jua kwa kiwango cha kuhakiki wakati wanaodai, wakachelewesha kufuturu, na wakawahisha daku, na wakaenda kinyume na sunna, na kwa hilo kheri kwao zikapungua, na zikakithiri kwao shari, tunamuomba Allah msaada.

التصنيفات

Sunnah za Funga.