إعدادات العرض
Atakayesahau hali yakuwa kafunga akala au akanywa, basi atimize swaumu yake, kwani Mwenyezi Mungu kamlisha na kamnywesha
Atakayesahau hali yakuwa kafunga akala au akanywa, basi atimize swaumu yake, kwani Mwenyezi Mungu kamlisha na kamnywesha
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayesahau hali yakuwa kafunga akala au akanywa, basi atimize swaumu yake, kwani Mwenyezi Mungu kamlisha na kamnywesha".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Hausa Português Kurdî සිංහල Tiếng Việt অসমীয়া ગુજરાતીالشرح
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayekula au kunywa kwa kusahau akiwa kafunga swaumu ya faradhi au sunna basi atimize swaumu yake wala asifungue; kwa sababu hakukusudia kufungua, bali hiyo ni riziki Mwenyezi Mungu kamsogezea na akamlisha na kumnywesha.فوائد الحديث
Kukubalika kwa swaumu ya aliyekula au kunywa kwa kusahau.
Hana dhambi aliyesahau akala au kunywa; kwa sababu hilo si kwa maamuzi yake.
Upole wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake na kuwafanyia wepesi juu yao na kuwaondolea tabu na uzito juu yao.
Hafungui mfungaji kwa chochote katika vile vyenye kufunguza ila zikikamilika sharti tatu: Ya kwanza: Awe anajua, akiwa mjinga hafungui, ya pili: Awe na kumbukumbu, kama kasahau swaumu yake ni sahihi na wala halazimiki kulipa, ya tatu: Iwe kwa hiari yake, na si kwa kulazimishwa, yaani atumie vyenye kufunguza kwa hiari yake mwenyewe.
التصنيفات
Vyenye kuharibu Funga.