إعدادات العرض
Swala ya mtu katika jamaa inazidi swala yake sokoni kwake na nyumbani kwake kwa daraja zaidi ya ishirini
Swala ya mtu katika jamaa inazidi swala yake sokoni kwake na nyumbani kwake kwa daraja zaidi ya ishirini
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Swala ya mtu katika jamaa inazidi swala yake sokoni kwake na nyumbani kwake kwa daraja zaidi ya ishirini, na hii ni pale mmoja wao atakapo tawadha na akaufanya vizuri udhu, kisha akaenda msikitini hakusudii kwa kwenda kwake ila swala, hakuna kinachomnyanyua isipokuwa swala, basi hatopiga hatua yoyote isipokuwa atanyanyuliwa daraja kwa hatua hiyo, na atasamehewa makosa kwa hatua hiyo mpaka atakapoingia msikitini, na anapoingia msikitini huhesabika kuwa yuko ndani ya swala madamu swala ndio bado inayomzuia kutoka, na Malaika humuombea rehema mmoja wenu madamu akiwa bado kakaa mahala aliposwali, wakisema: Ewe Mola wetu muhurumie, Ewe Mola wetu msamehe, Ewe Mwenyezi Mungu mkubalie msamaha wake, wanaendelea kufanya hivyo kwa muda atakaokuwa hajafanya maudhi yoyote, na madam hajatengua udhu".
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Hausa Kurdî Português සිංහල Svenska ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Tiếng Việt پښتو অসমীয়া دری Кыргызча or Malagasy नेपाली Čeština Oromoo Română Nederlands తెలుగు മലയാളം ไทย Српски Kinyarwanda ಕನ್ನಡ Lietuvių Shqip Wolof Українська ქართული Moore Magyarالشرح
Anaeleza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakaposwali muislamu katika jamaa, swala yake hiyo itakuwa bora kuliko swala yake nyumbani kwake au sokoni kwake kwa zaidi ya mara ishirini. Kisha akaeleza sababu ya hilo: Nayo nikuwa mtu atakapotawadha akatimiza vizuri udhu na ukaufanya vizuri, kisha akatoka kwenda Msikitini hakuna kinachomtoa ila kukusudia kusali, hatopiga hatua yoyote isipokuwa atanyanyuliwa kwa hatua hiyo daraja na nafasi ya juu, na hufutiwa kwake kwa hatua hiyo makosa, Atakapoingia Msikitini na akakaa akisubiri swala, basi atapata malipo ya swala na thawabu zake kwa muda wote atakaokaa akisubiri swala, na Malaika wakimuombea akiwa katika kikao chake aliposwalia, wakisema: "Ewe Mwenyezi Mungu msamehe, ewe Mwenyezi Mungu muhurumie, ewe Mwenyezi Mungu mfutie makosa" Huendelea kumuombea madam hajaharibu udhu wake, au akafanya yanayowakera watu au Malaika.فوائد الحديث
Swala ya mtu mmoja nyumbani kwake au sokoni kwake ni sahihi, lakini atapata dhambi kwa kuacha swala ya jamaa bila udhuru.
Swala ya jamaa Msikitni ni bora kuliko swala ya mtu peke yake kwa daraja ishirini na tano au sita.
Miongoni mwa kazi za Malaika ni kuwaombea waumini.
Ubora wa kwenda Msikitni pamoja na udhu.