Atakayekula kitunguusaumu, au kitunguu maji, basi na ajitenge nasi, au ajitenge na msikiti wetu, na akae nyumbani kwake

Atakayekula kitunguusaumu, au kitunguu maji, basi na ajitenge nasi, au ajitenge na msikiti wetu, na akae nyumbani kwake

Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayekula kitunguusaumu, au kitunguu maji, basi na ajitenge nasi, au ajitenge na msikiti wetu, na akae nyumbani kwake", Nakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliletewa chungu kikiwa na mbogamboga, akakuta zinaharufu, akauliza akaelezwa kilichomo katika mboga hizo, akasema: Wapewe baadhi ya Maswahaba zake aliokuwa nao, alipoiona hakupendezwa nayo, akasema: "Kula kwani mimi ninanong'ona na yule usiyenong'ona naye".

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim kwa riwaya zake]

الشرح

Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayekula kitunguu saumu au kitunguu maji asije msikitini, ili asiwaudhi ndugu zake katika wale wanaohudhuria swala ya jamaa kwa harufu yake, nalo ni katazo la kiusafi la kutokuja msikitini, na si katazo la kula; kwa sababu ni katika vyakula vya halali, na aliletewa Mtume rehema na amani ziwe juu yake chungu kikiwa na mbogamboga, aliponusa ndani yake harufu au alipoambiwa kilichomo, alikataa kula, na akakisogeza kwa baadhi ya Maswahaba zake akasema: Kula; kwani mimi husema na Malaika kwa wahyi. Na akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Malaika hukereka na harufu mbaya, kama wanavyokereka watu kwa harufu hiyo.

فوائد الحديث

Katazo la kuja msikitini kwa atakayekula kitunguu saumu, au kitunguu maji, au chochote chenye harufu mbaya.

Inaunganishwa na mambo haya, kila chenye harufu mbaya kinachowakera wenye kuswali, kama harufu ya sigara na tumbaku ugoro na mfano wa hivyo.

Sababu ya kukatazwa ni harufu, ikiondoka kwa kupikwa sana au kwa kinginecho; basi chukizo litaondoka.

Chukizo la kula vitu hivi kwa mwenye ulazima wa kuhudhuria swala msikitni; ili jamaa isimpite msikitini, madam hajavila kwa hila ya kukwepa kuhudhuria swala ya jamaa, hapa itakuwa ni haramu.

Mtume rehema na amani ziwe juu yake kukataa kula kitunguu saumu na mfano wake, si kwa ajili ya kuharamisha, bali ni kwa sababu ya mazungumzo yake na Jibril amani iwe juu yake.

Uzuri wa mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kiasi kwamba hukumu anaiambatanisha na sababu yake; ili mkusudiwa atulizane kwa kujua hekima.

Amesema Al-qadhi: Na wanachuoni wametumia kipimo hiki kwa maeneo yote yanayowakusanya watu kwa ajili swala kama viwanja vya Idd na jeneza na mfano wake katika sehemu zinazowakusanya watu kwa ajili ya ibada, na vile vile sehemu wanazokusanyika kwa ajili ya elimu na kumtaja Mwenyezi Mungu na sherehe mbali mbali na mfano wake, isipokuwa masoko na mfano wake hayaingii hapa.

Wamesema wanachuoni: Na katika hadithi hii kuna dalili ya kukataza kula kitunguu saumu na mfano wake wakati wa kuingia msikitini, hata kama pakiwa hakuna mtu ndani yake, kwa sababu ni mahala pa Malaika, na kwa ujumla wa maelekezo ya hadithi.

التصنيفات

Ubora wa Swala ya Jamaa na Hukumu zake.