Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni sita" Pakasemwa: Na ni zipi hizo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?, akasema: "Ukikutana naye msalimie, na akikuita muitikie, na akikutaka nasaha mnasihi, na akipiga chafya akamhimidi Mwenyezi Mungu basi muombee dua ya rehema, na akiugua mtembelee, na…

Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni sita" Pakasemwa: Na ni zipi hizo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?, akasema: "Ukikutana naye msalimie, na akikuita muitikie, na akikutaka nasaha mnasihi, na akipiga chafya akamhimidi Mwenyezi Mungu basi muombee dua ya rehema, na akiugua mtembelee, na akifariki msindikize

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni sita" Pakasemwa: Na ni zipi hizo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?, akasema: "Ukikutana naye msalimie, na akikuita muitikie, na akikutaka nasaha mnasihi, na akipiga chafya akamhimidi Mwenyezi Mungu basi muombee dua ya rehema, na akiugua mtembelee, na akifariki msindikize".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa miongoni mwa haki za muislamu juu ya ndugu yake muislamu ni mambo sita: La kwanza: Amsalimie akikutana naye kwa kusema: Assalaam alaikum, naye atajibu salamu kwa kusema: Waalaikumussalaam. La pili: Kuitika wito wake atakapomuita kwa ajili ya sherehe ya harusi au nyingineyo. La tatu: Kumpa nasaha akizihitajia, na wala usimsifie bure, au kumfanyia udanganyifu. La nne: Akipiga chafya akasema: Alhamdulillaah, basi muombee dua kwa kusema: Yar-hamkallaah (Akuhurumie Mwenyezi Mungu), naye ajibu kwa kusema: Yah-diikumullaahu wayuslih baalakum (Akuongozeni Mwenyezi Mungu na kutengenezeeni hali zenu). La tano: Akamuone na amtembelee atakapougua. La sita: Amswalie atakapofariki, na alisindikize jeneza lake mpaka azikwe.

فوائد الحديث

Amesema Shaukani: Na makusudio ya kauli yake: (Haki za muislamu) Nikuwa haitakiwi kuziacha, na kunakuwa kuzifanya kwake ima ni wajibu au sunna iliyotiwa mkazo inayofanana na wajibu ambayo haitakikani kuiacha.

Kujibu salamu ni faradhi ya lazima, mwenye kusalimiwa atakapokuwa mmoja, na wakiwa wengi basi mmoja anatosheleza, ama kuanza salamu asili yake ni sunna.

Mgonjwa kutembelewa ni katika haki zake juu ya ndugu zake waislamu; kwa sababu humuingizia furaha na liwazo ndani ya moyo wake, na ni faradhi ya kujitosheleza, wakifanya wenye kutosheleza basi wengine hawana dhambi.

Uwajibu wa kuitika wito kukiwa hakuna madhmbi ndani yake; ikiwa ni wito wa sherehe ya harusi basi jopo la wanachuoni wamesema kuwa ni wajibu kuitika, isipokuwa kukiwa na udhuru wa kisheria, ama ikiwa si sherehe ya harusi jopo la wanachuoni wakasema kuwa ni sunna.

Kumuombea dua aliyepiga chafya ni wajibu juu ya yule aliyesikia kumhimidiwa Mwenyezi Mungu mpiga chafya.

Ukamilifu wa sheria na pupa yake katika kuunganisha nguvu na umoja wa jamii na imani, na nyenzo za mapenzi kati ya mtu mmoja mmoja.

"Muombee rehema" Yaani kumuombea dua ya kheri na baraka, na tashmiiti (kumuombea dua) imesemekana maana yake: Mwenyezi Mungu akuweke mbali na kuchekwa na maadui, na ayaweke mbali nawe yale yatakayofanya adui yako akucheke, na tasmiit (kwa siin): Maana yake: Mwenyezi Mungu akuongoze katika ustaarabu ulionyooka.

التصنيفات

Hukumu za Kupenda na Kuchukia., Adabu ya kupiga Chafya na Miayo.