Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo kinga ya jambo langu

Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo kinga ya jambo langu

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo kinga ya jambo langu, na unitengenezee dunia yangu ambayo kunapatikana maisha yangu, na unitengenezee Akhera yangu ambako kunapatikana kuishi kwangu milele, na unijalie ziada ya uhai kwenye kila lenye heri, na ujalie kifo ni kitulizo changu kutokana na kila shari"

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Aliomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa dua iliyokusanya ndani yake misingi ya tabia njema alizotumwa kuzitimiliza; nazo ni kutengenezewa dini, na dunia, na Akhera, akachota kutoka katika matamshi haya mafupi kutengemaa kwa mambo makubwa matatu, na akaanza na kutengemaa kwa dini, ambayo ndiyo sababu ya kutengemaa hali ya Dunia na Akhera, akasema: "Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu" Kwa kuniafikisha kusimamia adabu zake kwa namna iliyokamilika na kutimia zaidi. "Ambayo ndiyo ngome ya jambo langu" Na iwe hifadhi kwa mambo yangu yote, ikiwa dini yangu itaharibika basi yataharibika mambo yangu, na nitapata hasara na kutoka patupu, na kwakuwa hakuwezi kutimia kutengemaa kwa dini inayotakiwa isipokuwa kwa kutengemaa dunia, akasema: "Na unitengenezee dunia yangu" Kwa kunipa afya ya mwili na amani, na riziki, na mke mwema, na kizazi kizuri na yale ninayoyahitaji, na yawe ya halali, na yanisaidie katika kukutii, kisha akataja udhuru katika kuomba kwake kutengemaa kwake; kwa kusema: "Ambayo kuna maisha yangu" Na mahala pa kuishi kwangu na muda wa uhai wangu. "Na unitengenezee Akhera yangu ambayo ndiyo marejeo yangu" Na kurejea kwangu ili kukutana na wewe, na hii ni kwa kutengemaa kwa matendo, na Mwenyezi Mungu kumuwezesha mja katika ibada na ikhlasi, na kuupata mwisho mwema. Na akapangilia rehema na amani ziwe juu yake Akhera baada ya dunia; kwa sababu ya kwanza ndio sababu ya kutengemaa ya pili, atakayekuwa na msimamo katika dini yake kwa namna atakavyo Mwenyezi Mungu, basi Akhera yake itanyooka na atapata furaha ndani yake. "Na uufanye uhai" Yaani: Na kurefushwa kwa umri "Kuwa ni ziada kwangu katika kila kheri" Ili nizidishe amali njema, "Na uyafanye mauti" na kuharakishwa kwake "Raha kwangu kutokana na kila shari" Na fitina na mitihani na majaribu kwa maasi na kughafilika, na ili iwe ni sababu ya kuepukana na matatizo ya Dunia na shida zake, na kupatikana kwa raha.

فوائد الحديث

Dini ndio kitu muhimu; na ndio maana alianza nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika dua.

Dini ndio ngao ya mwanadam inayomkinga dhidi ya kila shari.

Kuomba mambo ya kidunia kwa ajili ya kutengeneza dini na Akhera.

Si vibaya kutamani kufa kwa kuhofia mitihani na fitina katika dini, au kumuomba Mwenyezi Mungu kufa katika shahada.

التصنيفات

Dua zilizopokelewa toka kwa mtume.