Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba unipe afya katika Dunia na Akhera

Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba unipe afya katika Dunia na Akhera

Imepokelewa kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiacha dua hizi, kila anaposhinda jioni na kila anapoamka: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba unipe afya katika Dunia na Akhera, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba msamaha na afya katika dini yangu na dunia yangu na familia yangu na mali yangu, ewe Mwenyezi Mungu sitiri uchi wangu -Au aibu zangu- na utie amani yote ninayoyahofia, ewe Mwenyezi Mungu nihifadhi toka mbele yangu, na nyuma yangu, na kuliani kwangu, na kushotoni kwangu, na juu yangu, na ninajilinda kwa utukufu wako nisijekuvamiwa tokea chini yangu".

[Sahihi]

الشرح

Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiacha maombi haya pindi anaposhinda jioni na pindi anapoamka. "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba afya" na kusalimika na magonjwa na mabalaa na shida za dunia, na matamanio na fitina za kidunia "Katika dunia na Akhera" kwa au kwa baadae "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba msamaha" na kusalimika na aibu, "Katika dini yangu" kutokana na ushirikina na uzushi na maasi, "na dunia yangu" katika majanga na kero na shari, "na familia yangu" mke wangu na wanangu na ndugu zangu, "na mali yangu" na mali zangu na matendo yangu. "Ewe Mwenyezi Mungu sitiri uchi wangu" Yaani: Na yale yaliyokwangu katika aibu na dosari na mapungufu na ufute dhambi zangu, "na utie amani hofu yangu" Mfadhaiko wangu na hofu yangu. "Ewe Mwenyezi Mungu nihifadhi" Na uzuie kwangu balaa miongoni mwa yale yenye kuudhi na mabalaa, "mbele yangu na nyuma yangu, na kuliani kwangu, na kushotoni kwangu, na juu yangu" Kiasi kwamba aliomuomba Mwenyezi Mungu amuhifadhi kutoka pande zote; kwa sababu mabalaa na maafa humfika mtu na kumuelekea kutoka moja kati ya pande hizi. "Na ninajilinda kwa utukufu wako nisijekuvamiwa" na nisichukuliwe hatua toka chini yangu ghafla, nikaangamia ghafla "kutoka chini yangu" nikaangamia kwa kudidimizwa.

فوائد الحديث

Kudumu na maneno haya kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Mwanadam kama alivyo anaamrishwa kumuomba Mwenyezi Mungu afya katika dini, vile vile kaamrishwa kumuomba katika dunia.

Amesema Attwayibi: Imekusanya pande zote sita; kwa sababu maafa mengi hutokea katika pande hizo, na akatia mkazo katika upande wa chini kwa sababu maafa ya kutoka chini huwa mabaya zaidi.

Kilicho bora wakati wa kusoma Adhkari, wakati wa asubuhi: Ni kuanzia kuchomoza kwa Alfajiri mpaka kuchomoza Jua mwanzo wa mchana, na kuanzia baada ya Lasiri mpaka kabla ya Maghribi, ikiwa atasema baada ya wakati huo, yaani: Akazisoma asubuhi baada ya Jua kunyanyuka itafaa pia, na hata akisema baaada ya Adhudhuri itamfaa pia, na ikiwa atazazisema baada ya Maghrib itamtosheleza pia, huo ndio wakati wa kufanya dhikri.

Dalili ikionyesha kuwa dhikri inamuda maalum wakati wa usiku kama kusoma aya mbili za mwisho katika suratul baqara basi hii inakuwa ni baada ya kuzama kwa Jua.

التصنيفات

Dua zilizopokelewa toka kwa mtume.