Mwanamke yeyote atakayeolewa bila idhini ya walii wake, basi ndoa yake ni batili" Akasema hivyo mara tatu "Ikiwa atamuingilia basi mahari yake ndio itakuwa kwa ajili ya kile alichokifanya kwake, na ikiwa watazozona basi kiongozi ndiye msimamizi wa asiyekuwa na msimamizi

Mwanamke yeyote atakayeolewa bila idhini ya walii wake, basi ndoa yake ni batili" Akasema hivyo mara tatu "Ikiwa atamuingilia basi mahari yake ndio itakuwa kwa ajili ya kile alichokifanya kwake, na ikiwa watazozona basi kiongozi ndiye msimamizi wa asiyekuwa na msimamizi

Kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mwanamke yeyote atakayeolewa bila idhini ya walii wake, basi ndoa yake ni batili" Akasema hivyo mara tatu "Ikiwa atamuingilia basi mahari yake ndio itakuwa kwa ajili ya kile alichokifanya kwake, na ikiwa watazozona basi kiongozi ndiye msimamizi wa asiyekuwa na msimamizi".

[Sahihi]

الشرح

Alitahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwanamke kujiozesha mwenyewe pasina idhini ya walii wake, nakwamba ndoa yake ni batili, na hilo alilikariri mara tatu, kana kwamba haijatendeka. Akimuingilia huyu aliyemuoa pasina idhini ya walii wake; hapo mahari kamili itakuwa ni haki yake, kwa lile tendo la ndoa alilolipata katika tupu yake. Kisha wakizozana mawalii kuwa ni nani mwenye haki ya kufungisha ndoa (na daraja zao zikawa ni sawa) ndoa itafungishwa na yule atakayetangulia miongoni mwao, ikiwa huyu anamtazamo mzuri katika masilahi ya mwanamke huyo, walii akikataa kumuozesha basi hapa mwanamke atakuwa ni sawa nakwamba hana walii; hapa kiongozi au kadhi na mfano wao ndio watakuwa mawalii wake, na vinginevyo hakuna uwalii wa kiongozi anapokuwepo walii.

فوائد الحديث

Sharti la kuwa na walii ili kusihi ndoa, na ilielezwa kutoka kwa bin Mundhir kuwa hakuna Swahaba aliyeripotiwa kupingana na hilo.

Katika ndoa batili mwanamke anastahiki mahari kwa sababu ya kuingiliwa.

Kiongozi ni walii wa yule asiyekuwa na walii katika wanawake, sawa sawa hilo liwe kwa sababu ya kutokuwepo kwake kabisa, au kwa sababu ya kukataa kumuozesha.

Kiongozi anazingatiwa kama walii kwa asiyekuwa na walii, katika hali ya kukosekana kwa walii au kushindika kuwepo, na atasimama kadhi badala yake; kwa sababu yeye ndiye mbadala wake katika maswala kama haya.

Uwalii kwa mwanamke haumaanishi kuwa mwanamke hana haki, bali ana haki, na haifai kwa walii wake kumuozesha ila kwa idhini yake.

Sharti za ndoa sahihi: Ya kwanza: Kuwaainisha wote wawili, kwa ishara au kwa kuwataja majina au sifa na mfano wake, ya pili: Kuridhia kutoka kwa wote wawili, ya tatu: Mwanamke afungishwe ndoa na walii wake, ya nne: Ndoa iwe na mashahidi.

Ni sharti kwa walii anayefungisha ndoa: Kwanza awe na akili, la pili: Awe mwanaume, la tatu: Kubalehe, kwa kufikisha kwake umri wa miaka kumi tano, au kwa kujiotea, la nne: Dini iwe moja, hakuna uwalii wa kafiri kwa muislamu wa kiume au wa kike, na vile vile hakuna uwalii wa muislamu kwa kafiri mwanaume au mwanamke, la tano: Uadilifu unaopingana na uovu, na inatosha katika hilo kutazama masilahi ya yule anayesimamia kumuozesha, la sita: Walii awe mwerevu asiwe mpumbavu, nao ni uwezo wa kujua ni nani anayeendana na anayemuozesha, na masilahi ya ndoa.

Wanachuoni wameweka taratibu za walii kumuozesha mwanamke, haifai kumvuka walii wa karibu isipokuwa wakati wa kukosa kwake sharti, na walii wa mwanamke ni baba yake, kisha wapewa usia wake, kisha babu yake wa upande wa baba na kwenda juu, kisha mwanaye wa kiume, kisha wajukuu zake na kuendelea, kisha kaka yake wa baba na mama, kisha kaka yake wanayechangia baba, kisha watoto wao, kisha baba zake wadogo au wakubwa wa baba na mama mmoja wa baba yake, kisha ami yake wa upande wa baba, kisha watoto wao, kisha ndugu wa karibu kisha anayefuata katika ukoo kama ilivyo katika mirathi, na kiongozi muislamu na anayekaa badala yake kama kadhi ni walii kwa asiyekuwa na walii.

التصنيفات

Ndoa.