Sharti zenye haki zaidi kwenu nyinyi kuzitekeleza ni zile mlizohalalishia tupu

Sharti zenye haki zaidi kwenu nyinyi kuzitekeleza ni zile mlizohalalishia tupu

Imepokewa kutoka kwa Uqbah Bin Aamir -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake: "Sharti zenye haki zaidi kwenu nyinyi kuzitekeleza ni zile mlizohalalishia tupu".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa sharti bora kabisa kwa kutekelezwa ni zile zilizokuwa sababu ya uhalali wa kustarehe na mwanamke, nazo ni zile sharti za halali anazozitaka mwanamke wakati wa kufunga ndoa.

فوائد الحديث

Uwajibu wa kutekeleza sharti ambazo amezitilia umuhimu mmoja kati ya wanandoa wawili kwa mwenzie, isipokuwa sharti itakayoharamisha halali au kuhalalisha haramu.

Kutekeleza sharti za ndoa kumetiliwa mkazo kuliko sharti zote; kwa sababu huambatana na kuhalalisha tupu.

Ukubwa wa nafasi ya ndoa katika Uislamu, kiasi ambacho umetilia mkazo juu ya kutimiza sharti zake.

التصنيفات

Masharti ya Ndoa