إعدادات العرض
Kwa hakika Mwenyezi Mungu anapenda ichukuliwe ruhusa yake katika kufanya yaliyo mepesi, kama vile anavyopendelea kwa waja wake kufanya mambo yake aliyowawajibishia kuyafanya
Kwa hakika Mwenyezi Mungu anapenda ichukuliwe ruhusa yake katika kufanya yaliyo mepesi, kama vile anavyopendelea kwa waja wake kufanya mambo yake aliyowawajibishia kuyafanya
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kwa hakika Mwenyezi Mungu anapenda ichukuliwe ruhusa yake katika kufanya yaliyo mepesi, kama vile anavyopendelea kwa waja wake kufanya mambo yake aliyowawajibishia kuyafanya".
[Sahihi] [Imepokelewa na Ibnu Hibaan]
الترجمة
العربية English မြန်မာ Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands اردو Español Bahasa Indonesia ئۇيغۇرچە বাংলা Türkçe Bosanski සිංහල हिन्दी Tiếng Việt Hausa മലയാളം తెలుగు ไทย پښتو অসমীয়া Shqip دری Ελληνικά Български Fulfulde Italiano ಕನ್ನಡ Кыргызча Lietuvių Malagasy or Română Kinyarwanda Српски тоҷикӣ O‘zbek नेपाली Moore Kurdî Oromoo Wolof Soomaali Français Tagalog Azərbaycan Українська bm தமிழ் Deutsch ქართული Português Македонски Magyar فارسی Русский 中文الشرح
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: kuwa Mwenyezi Mungu anapenda ziendewe ruhusa zake ambazo ameziweka, ikiwemo kufanya wepesi katika hukumu na ibada, na kufanya wepesi kwenye ibada kwa aliyekalifishwa na sheria ikiwa ni kwa dharura- kama vile kupunguza swala na kuikusanya wakati wa safari. Kama ambavyo Mwenyezi Mungu anapenda yafanywe mambo yake ya wajibu, kwa sababu amri ya Mwenyezi Mungu katika kufuata ruhusa na kutekeleza wajibu yote ni sawa.فوائد الحديث
Huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na kuwa yeye Mwenyezi Mungu aliyetakasika na machafu anapenda ruhusa yake ifanyiwe kazi.
Ukamilifu wa sheria hii, na kuondosha kwake uzito kwa waislamu.