Hakitosimama kiyama mpaka zama zikaribiane

Hakitosimama kiyama mpaka zama zikaribiane

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Sala na amani ziwe juu yake-: "Hakitosimama kiyama mpaka zama zikaribiane, mwaka utakuwa kama mwezi, na mwezi utakuwa kama wiki, na wiki kama siku, na siku kama saa, na saa itakuwa kama kuungua kwa jani kavu la mtende".

[Sahihi] [Imepokelewa na Ahmad]

الشرح

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa miongoni mwa alama za Kiyama ni kukaribiana zama. Mwaka utapita kama mwezi unavyopita, Na mwezi utapita kama inavyopita wiki, Na wiki itapita kama inavyopita siku. Na siku itapita kama inavyopita saa moja, Na saa itapita upesi kama linavyochomwa jani kavu la mtende.

فوائد الحديث

Miongoni mwa alama za Kiyama ni kushuka kwa baraka katika zama au uharaka wake.

التصنيفات

Maisha ya Barzakhi(Baada ya kufa)