Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akimtaja Allah katika nyakati zake zote

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akimtaja Allah katika nyakati zake zote

Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akimtaja Allah katika nyakati zake zote.

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy, ameiwekea maelezo kwa njia ya mkato]

الشرح

Anaeleza Aisha mama wa waumini -Radhi za Allah ziwe juu yake- kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa na pupa kubwa ya kumtaja Allah Mtukufu, nakuwa yeye alikuwa akimtaja Allah Mtukufu katika nyakati zote mahala popote na katika hali zote.

فوائد الحديث

Hakuna sharti la twahara ya hadathi ndogo na kubwa kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akidumu na kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Himizo la kukithirisha kumja Mwenyezi Mungu Mtukufu katika nyakati zote kwa kumuiga Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, isipokuwa katika hali ambazo zinakatazwa ndani yake kufanya hivyo, kama kukidhi haja.

التصنيفات

Hukumu za Qur'an na Misahafu.