إعدادات العرض
Hassan na Hussein ni mabosi wa vijana wa peponi
Hassan na Hussein ni mabosi wa vijana wa peponi
Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hassan na Hussein ni mabosi wa vijana wa peponi".
الترجمة
العربية Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский 中文 हिन्दी اردو Hausa Kurdî Português Nederlands Tiếng Việt অসমীয়া ગુજરાતી አማርኛ پښتو සිංහල ไทยالشرح
Alieleza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake kuwa wajukuu zake Hassan na Hussein watoto wa Ally bin Abii Twalib na Fatma binti wa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake na Allah amridhie, wao ni mabosi katika fadhila wa kila aliyekufa akiwa kijana na akaingia peponi, au wao ni mabosi wa vijana wa watu wa peponi, kasoro Manabii na Mahalifa (viongozi) waongofu.فوائد الحديث
Hapa kuna fadhila za wazi za Hassan na Hussein radhi za Allah ziwe juu yao.
Imesemekana katika maana ya hadithi kuwa: Wao wakati wa kuzungumzwa hadithi hii walikuwa ndio mabosi wa vijana wa wale miongoni mwao watakaokuwa katika watu wa peponi katika vijana wa zama hizi, au wao ni bora kuliko yule ambaye fadhila zake hazijathibiti kwa ujumla kama Manabii na Mahalifa (viongozi), au wao ni mabosi wa kila mwenye kusifika na sifa ya ujana, kama murua (heshima) na ukarimu na ushujaa, na haukutajwa umri maalumu wa ujana; kwa sababu Hassan na Hussein walikufa wakiwa watu wazima.