إعدادات العرض
Litafikia jambo hili ulipofika usiku na mchana, na wala hatoacha Mwenyezi Mungu nyumba ya mjini wala ya kijijini isipokuwa ataiingiza Mwenyezi Mungu dini hii
Litafikia jambo hili ulipofika usiku na mchana, na wala hatoacha Mwenyezi Mungu nyumba ya mjini wala ya kijijini isipokuwa ataiingiza Mwenyezi Mungu dini hii
Imepokelewa kutoka kwa Tamim Ad-Dari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Litafikia jambo hili ulipofika usiku na mchana, na wala hatoacha Mwenyezi Mungu nyumba ya mjini wala ya kijijini isipokuwa ataiingiza Mwenyezi Mungu dini hii, kwa utukufu wa yeyote au kwa udhalili wa yeyote, ni utukufu anaoutukuza Mwenyezi Mungu uislamu, na ni udhalili anaoudhalilisha Mwenyezi Mungu ukafiri" na alikuwa Tamimu Dari akisema, nililijua hilo kwa watu wa familia yangu, kwa hakika alipata aliyesilimu miongoni mwao kheri na heshima na utukufu, na aliyekuwa kafiri alipata udhalili na unyonge na ulipaji kodi.
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Türkçe اردو हिन्दी Tagalog 中文 Kurdî Português Русский دری অসমীয়া Tiếng Việt አማርኛ Svenska ไทย Yorùbá Кыргызча ગુજરાતી Hausa नेपाली Română മലയാളം Nederlands Oromoo සිංහල پښتو తెలుగు Soomaali Kinyarwanda Malagasy ಕನ್ನಡالشرح
Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani zimshukie, amesema kuwa dini hii itaenea sehemu zote za ardhi, hivyo dini hii itafika sehemu yoyote ile ufikapo usiku na mchana, na hatoiwaacha Mwenyezi Mungu Mtukufu nyumba yoyote mijini na vijijini wala mabondeni na majangwani isipokuwa ataiingiza dini hii, atakayeikubali dini hii na akaiamini basi atakuwa mtukufu kwa sababu ya utukufu wa Uislamu, na atakayeikataa na akaipinga basi atakuwa dhalili mwenye kufedheheshwa. Kisha swahaba Tamim Al-Dari, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, akaeleza kuwa alilijua hilo aliloambiwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake kwa watu nyumba yake hasa, kwani kila aliyesilimu miongoni mwao alipata kheri na heshima, na utukufu, na aliyekufuru miongoni mwao alipata udhalili na unyonge, hii ikiwa ni pamoja na pesa anazowalipa Waislamu kama Jizia (Kodi).فوائد الحديث
Habari njema kwa waislamu kuwa dini yao itasambaa katika pande zote za Ardhi.
Utukufu ni kwa Uislamu na waislamu na udhalili ni kwa makafiri na ukafiri.
Kuna dalili miongoni mwa dalili za utume na alama miongoni mwa alama zake, kiasi kwamba jambo hilo limetokea kama alivyoeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
التصنيفات
Alama za Kiama .