إعدادات العرض
Mwenye kwenda upesi kuwasaidia wajane na maskini ni kama mwenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, au mwenye kusimama usiku na kufunga mchana
Mwenye kwenda upesi kuwasaidia wajane na maskini ni kama mwenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, au mwenye kusimama usiku na kufunga mchana
Kutoka kwa Abuu Huraira amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Mwenye kwenda upesi kuwasaidia wajane na maskini ni kama mwenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, au mwenye kusimama usiku na kufunga mchana"
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español فارسی Français Bahasa Indonesia Русский Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी Kurdî Hausa Português മലയാളം తెలుగు தமிழ் မြန်မာ Deutsch 日本語 پښتو Tiếng Việt অসমীয়া Shqip Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá ئۇيغۇرچە සිංහල ไทย دری Кыргызча or Kinyarwanda नेपाली Română Lietuvių Malagasy ಕನ್ನಡ Oromoo Nederlands Soomaali Српски Українська Wolof Mooreالشرح
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwenye kusimamia masilahi ya mwanamke aliyefiwa na mumewe na ikawa hakuna yeyote mwenye kusimamia mambo yake, na masikini muhitaji, na akawapa matumizi akitaraji malipo mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi mtu huyu katika malipo ni kama mpigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na ni kama mwenye kusimama katika swala ya tahajudi asiyechoka, na mfungaji asiyefungua.فوائد الحديث
Himizo la kusaidizana na kuhurumiana na kutatua haja za watu madhaifu.
Ibada inakusanya kila amali njema, na miongoni mwa ibada ni kwenda haraka kuwasaidia wajane na masikini.
Amesema Bin Hubaira: Na makusudio yake hapa nikuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu humkusanyia thawabu za mfungaji na msimamaji usiku kwa ajili ya ibada na mpigana Jihadi kwa mpigo mmoja; na hii ni kwa sababu amesimama na mjane nafasi ya mume wake..., na akasimama upande wa masikini aliyeshindwa kujimudu mwenyewe, akatoa hiki kilichozidi katika matumizi yake, na akatoa sadaka kwa kuikandamiza nafsi yake, ndio maana manufaa yake yakawa sawa na swaumu na kisimamo cha usiku na Jihadi.
التصنيفات
fadila za matendo ya viungo.