Mfano wa aliyesimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu na mwenye kuingia ndani yake, ni kama mfano wa watu waliotengeneza boti (safina)

Mfano wa aliyesimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu na mwenye kuingia ndani yake, ni kama mfano wa watu waliotengeneza boti (safina)

Kutoka kwa Nuumaan bin bashiri Radhi za Allah ziwe juu yao, kutoka kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Mfano wa aliyesimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu na mwenye kuingia ndani yake, ni kama mfano wa watu waliotengeneza boti (safina), wakawa baadhi yao wako juu ya safina na wengine wako chini yake, na wakawa wale walioko chini yake wanapohitajia maji wanakwenda kwa wale walioko juu yao, wakasema: Lau kama tungetoboa katika sehemu yetu kitobo wala tusingewaudhi walioko juu yetu, ikiwa watawaacha watekeleze walilolikusudia wataangamia wote, na ikiwa watawashika na kuwazuia wataokoka na wataokoka wote".

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Mtume Rehema na amani ziwe juu yake amepiga mfano wa wale wenye kusimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu, wenye msimamo katika amri ya Mwenyezi Mungu, wenye kuamrisha mema na kukataza maovu, na mfano wa wenye kutumbukia katika mipaka ya Mwenyezi Mungu wenye kuacha mema, na kufanya maovu, na athari ya hilo katika kusalimika jamii, ni sawa na mfano wa watu waliopanda boti, wakagawana nafasi nani akae juu na nani akae chini ya boti, wengine wakapata nafasi ya kukaa juu na wengine wakapata nafasi ya kukaa chini, na wakawa hawa walioko chini wanapotaka kuchota maji wanakwenda kwa wale walioko juu yao, Kisha wale wa chini wakasema: Lau tungeli toboa tundu mahali petu chini ili tusiwaudhi walio juu yetu, basi lau walio juu wangewaacha kufanya hivyo, basi meli ingewazamisha wote, na lau wangeliwakataza na kuwazuia, makundi yote mawili yangeokoka.

فوائد الحديث

Umuhimu wa kuamrisha mema na kukataza maovu katika kuzihifadhi jamii na kusalimika kwake.

Miongoni mwa njia ya ufundishaji ni kupiga mifano, kwa ajili ya kusogeza uelewa wa akili kwa picha ya kitu chenye kueleweka.

Kufanya uovu kwa wazi na kuto kukemea madhara yake yanarudi katika jamii nzima.

Kuangamia kwa jamii kunaambatana na kuwaacha waovu wakiendelea kutapakaza maovu katika Ardhi.

Kufanya mambo kimakosa na nia ikawa njema hili halitoshi kurekebisha matendo.

Majukumu katika jamii ya kiislamu ni ya watu wote, hayaegemezwi kwa mtu maalum.

Kuadhibiwa kwa watu wote kwa sababu ya madhambi ya wachache, ikiwa hayatokemewa.

Waovu hudhihirisha maovu yao kwa sura ya kheri katika jamii kama walivyo wanafiki.

التصنيفات

7-fadhila na ubora wa kuamrisha Mema Na Kukataza Mabaya:, 7-fadhila na ubora wa kuamrisha Mema Na Kukataza Mabaya: